Apr 25, 2013

MADIWANI WAUJIA JUU WARAKA KUTOKA TAMISEMI, KISA KUZIBA MIANYA

Na Indaba africa writter

Katika hali inayoonyesha TAMISEMI kugusa maeneo oevu ya baadhi ya mabaraza ya madiwani nchini, hatua yake ya kutoa waraka wa shughuli za ukaguzi wa miradi kufanywa na kamati ya Fedha,Utawala na Mipango FMU imeonekana kuwa mwiba mchungu kwenye baraza la halmashauri ya Mbozi leo baada ya waheshimiwa madiwani kutaka kuazimia kinyume cha kanuni maelekezo kutoka ngazi za juu! story kamili inafuata----


 kutoka kushoto ni Makamu mwenyekiti ALAN MGULA, akifuatiwa na Mwenyekiti ERICK  AMBAKISYE na akifuatiwa na DED MBOZI Levison Chilewa

 michango ilianza hivi
 Hawa watunga sheria wa baraza la Mbozi wakiwa hewani kama hivyo wakati kikao kikiendelea
 Mh Emily Mzumbwe akichambua suala la uchangiaji wa hisa kwenye benki ya wananchi wa Mbozi ambapo limeonekana kurudisha reverse na madiwani baada ya kutaka mchakato huo usipelekwe puta kwa maelezo kuwa lazima wananchi waelimishwe pole pole namna ya kuchangia hisa zao badala ya kukata juu kwa juu sehemu ya fedha kwenye mauzo ya kahawa yao
 Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya MBOZI wakisikiliza  majadiliano
 Kulia wa kwanza ni katibu tawala Mbozi bwana Lazaro Mwankenja akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji Mbozi bwana Levison Chilewa wakifuatilia upepo unavyokwenda kwenye baraza hilo
 AFISA utumishi  Bwana Zabron Lulandala akifuatiwa na afisa Mipango wilaya bwana Ngoi wakifuatilia mijadala kwenye baraza la madiwani leo
 Baadhi ya watendaji kutoka ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Mbozi pamoja na ofisi ya mkuu wa wilaya wakifuatilia mijadala kwenye baraza hilo leo

Hali hiyo ilijitokeza baada ya madiwani kupitia kamati zao kuanza kulalamika hatua iliyofikiwa ya kuzuiwa kwenda kukagua miradi wakiwa kwenye kamati zao na badala yake kupewa maelezo kuwa kuna waraka unaozuia kamati hizo kutokana na kukosekana ufanisi!

Ndipo miongozo mwenyekiti, azimio na maneno mengine ilipoanza kusikika, lakini mwishowe ikawa ngumu kurudisha wwaraka huo TAMISEMI na badala yake madiwani kukubaliana nao kwa shingo upande

Hatua hiyo ilifikiwa\ baada ya ufafanuzi kutolewa kuwa kimsingi serikali za mitaa pamoja na kuwa ni muhimili muhimu katika kuunganisha wananchi na kuleta maendeleo haimaanishi kuwa serikali kuu haina nguvu ya kuelekeza jambo mbele ya serikali za mitaa.

Na kwamba kwa kutambua hilo ndiyo sababu halmashauri kwa sehemu kubwa kama siyo asilimia 95% hutegemea ruzuku kutoka serikali kuu, hivyo pale inapoagizwa baadhi ya mabadiliko ngazi za chini hakuna lugha ya kuyapamba maelekezo hayo bali kuyatekeleza

Ndipo diwani mmoja akasimama na kuomba mwongozo kisha akachomekea na azimio! hata hivyo mwenyekiti wa baraza hilo akatoa ufafanuzi kuwa serikali haiwezi kuazimiwa kwakuwa baraza hilo limeundwa pia kutokana na maelekezo na miongozo kutoka juu hivyo waheshimiwa wawe wapole kwanza!
katika hatua nyingine suala la uanzishwaji wa benki ya wananchi ya Mbozi leo limeendelea kupigwa dana dana ya kukubaliana kuto kubaliana! baada ya madiwani kuunga mkono kuanzishwa kwa benki hilo lakini wakitaka wananchi waleweshwe pole pole na pia wapate ziara ya kwenda kujifunza mikoa mingine namna ya benki hizo zinavyofanya kazi
Katika hali inayoonyesha kuwa wimbi hilo lilishawekwa mapema, kila aliyenyanyuka alikuwa akiongezea misumali ya kuzuia kuharakishwa kuchangisha shilingi 200 kwa kilo ya kahawa kwaajili ya uanzishaji wa benki hiyo ambapo baada ya maelezo ya ufafanuzi ya mkurugenzi mtendaji wilaya ya MBOZI, bado suala hilo liliamuliwa kwa kutakiwa kwanza wapewe ziara na baadaye wananchi waelimishwe namna bora ya kushiriki uanzishaji wa benki hiyo.
indabaafrica blog