Apr 3, 2013

MACHAFUKO YA TUNDUMA YAHAMIA ILEJE USIKU HUU

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI AKITAFAKARI JAMBO PAMOJA NA BAADHI YA ASKARTI POLISI MJINI TUNDUMA KUFUATIA VURUGU ILIYOIBULIWA LEO ASUBUHI JUU YA SAKATA LA UCHINJAJI KATI YA WAKRISTO NA WAISLAMU


BAADHI YA WANAHABARI WA MKOA WA MBEYA WAKIWA WAMEJIBANZA KATIKA KITUO CHA POLISI MJINI TUNDUMA KUEPUKA ADHA YA VURUGU ZILIZOIBUKA LEO ASUBUHI


 Taarifa  zilizoufikia mtandao wa Indabaafrica usiku huu zinaeleza kuwa baada ya tukio la mchana kutwa la vurugu katka mji wa Tunduma, mambo hayo hayo yamehamia wilayani Ilejea ambako askari wamepelekwa usiku huu kwenda kukabiliana  na vurugu hizo
 
Kulingana na taarifa hizo, vurugu zimezuka katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Ileje ambapo miji ya Isongole na Itumba pia kumezuka vurugu za uchomaji matairi barabarani na rabsha zilizosababisha kuomba nguvu zaidi kutoka Mbeya ambapo polisi waliokuwa operesheni ya Tunduma wamelazimika kugawanywa kwenda kutoa msaada zaidi
 
Aidha mkuu wa mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa viongozi waliofika mjini Tunduma kufuatilia kwa karibu tukio hilo na amekuwa akitoa maelekeozo namna ya kupunguza uwezekano wa matukio ya uhalifu na kutafuta ufumbuzi wa vurugu hizo
 
vyanzo vinadokeza kuwa bado katika mji wa Tunduma hali haijatengamaa vyema na kwamba ulinzi umeimarishwa na katika hatua nyingine magari ya IT yanavuka kwenda nchini zambia, kwa sehemu kubwa yamejazana katika barabara ya kuanzia mbeya hadi Mbozi-Vwawa  nje ya mji wa Tunduma kusubiria hali ya utulivu irejee vyema.
 
Akizungumza na indaba africa mmoja wa madereva amedokeza kuwa kutokana na hofu ya kutokea kwa uharibifu wa mali za watu, wamelazimika kupiga kambi nje ya mji wa Tunduma ili kusubiria kutulie na hatimaye kukabidhi magari hayo eneo la mpakani tayar kupelekwa kwenye nchi za Zambia na Kongo ambako ndiko wamiliki wapo
 
Hali hiyo imetajwa kuwaongezea gharama madereva hao kutokana na fedha walizolipwa kwa safari ya kufikisha gari eneo la Tunduma ambayo ni kati ya dola za kimarekani 50 hadi 100 imesababisha kula kwao kwakuwa wanachukua zaidi ya siku tatu, tofauti na matarajio ya safari zao kuchukua siku moja. 
ASKARI WA KIKOSI CHA MBWA WAKIJIANDAA KUKABILIANA NA LOLOTE KATIKA VURUGU HIZO




Gari la mtandao wa Mbeya yetu likiwa limebeba wanahabari waliofika mjini Tunduma kufuatilia tukio zima la vurugu katika mji huo




ASKARI POLISI MARA BAADA YA KUWATAWANYA WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI WAUMINI WA DINI YA KIKRISTO WALIOSHINIKIZA KUFUNGWA KWA MABUCHA YA WAISLAMU


 









picha  na habari hapa chini na Rashid Mkwinda

KUNDI la watu wanaosadikiwa kuwa ni waumini wa dini ya Kikristo wamevamia  kuvamia bucha za nyama zinazomilikiwa na waislamu na kulazimishwa kufungwa kwa bucha hizo kutokana na madai ya kuwekwa kwa uwiano sawa wa uchinjaji baina ya waislamu na wakristo.
Kundi hilo la waumini walikuwa wakipita katika barabara kadhaa za mji mdogo wa Tunduma kushinikiza kufunguliwa kwa mabucha ya wakristo na kuibua taharuki kwa baadhi ya wafanyabiashara wa maeneo hayo ambao walilazimika kufunga maduka baada ya askari kuanza kurusha mabomu kutawanya watu hao.
Vurugu hizo ambazo ziliambatana na vijana hao kuziba barabara na kuchoma matairi zilianza kutawanya kwa mabomu ya machozi ilhali kundi hilo la watu nalo lilianza kuwarushia mawe askari waliokuwemo kwenye magari ya doria na kusababisha askari mmoja aliyekuwa akiendesha gari la polisi kujeruhiwa.
Kutokana na hali hiyo mpaka wa Tanzania na Zambia ulilazimika kufungwa ili kupisha vurugu hizo ambazo zimedumu kuanzia saa 4;00 asubuhi mpaka majira ya saa 11 jioni.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani ambaye alifika kwenye eneo la tukio alisema kuwa vurugu hizo zinaonekana kuwa na ushawishi wa kisiasa kutokana na ukweli kuwa hazikupaswa kufikia hatua hiyo.
Kamanda Athumani amesema kuwa jeshi la polisi linawatafuta Mchungaji wa kanisa la KKKT la mjini Tunduma aliyefahamika kwa jina la Gidioni Mwamafupa na Diwani wa Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka kutokana na kudaiwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine juu ya kutokea kwa tukio hilo.
Amesema kuwa mbali na watu hao jeshi la polisi linawashikilia zaidi ya watu 40 ambao wanaendelea kusakwa kutokana na kusababisha vurugu hizo ambazo zimesababisha kukwamishwa kwa shughuli mbalimbali za kibiashara mjini humo.
Awali inadaiwa kuwa baadhi ya waumini wa dini ya Kikristo walipeleka barua kwenye uongozi wa serikali ya mji huo wakitaka wapewe ridhaa ya kuchinja kama vile ambavyo waumini wa dini ya kiislamu wanafanya.
Katika madai yao ambayo yalimfikia mkuu wa wilaya hiyo Abihudi Saideya walihitaji kupata kibali cha kuchinja ambapo hata hivyo kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya yalilikuwa yakifanyiwa kazi ngazi ya Taifa.
Amesema kuwa hata hivyo waumini hao walianza kuchinja kabla hawajapewa kibali cha serikali na kusababisha kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi baina ya waumini wa dini hizo.