Jun 23, 2013

KIMONDO YA MBOZI YAZIDI KUPETA LIGI YA MABINGWA RAUNDI YA PILI, YATOA SARE UGENINI MUSOMA

Timu ya Kimondo ya wilayani Mbozi imeendeleza wimbi la kujitengenezea mazingira mazuri kuingia ligi daraja la kwanza  Tanzania bara baada ya kuilazimisha sare ya bao 2-2 Timu ya Polisi Jamii ya Musoma katika uwanja wake wa Nyumbabi wa Karume mjini Msoma
Polisi jamii ambao walianza kupata bao lao la kwanza walijikuta wakishindwa kubana na badala yake wakaachia mnamo dakika ya 36 baada ya Kimondo kupanga mashambulizi huku wakiwasiliana kwa kutumia kiwemba, kindali na kinyiha huku wakiwaaacha maafande wakishangaa hadi Geofrey Mlau akiandika bao la kwanza na lakusawazisha.
Nyumbani ni nyumbani ilidhihirika baada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa nguvu sawa kwa kufungana bao moja kwa moja, kipindi cha pili kilianza kwa mashambulizi ya kasi kutoka polisi jamii ambao waliweza kupata bao la pili mnamo dakika ya 67 lakini halikudumu muda mrefu kwani mnamo dakika ya 75 hali ilikuwa mbaya kwa wenyeji
Alikuwa Imani Wilson aliyewainua mashabiki wa Musoma bila kujali uzalendo kwa timu yao na kuamua kushangilia timu ya wageni Kimondo SC baada ya kutungua shuti la kufa mtu lililomfanya mlindamlango wa Polisi Jamii kujifanya kama vile alikuwa akisikiliza simu kwa jinsi lilivyoingia na kumchanganya kabisaa.
Ikiongozwa na mlezi wao ERICK MINGA Kimondo iliendelea kufanya mashambulizi yenye lengo la kuwadharirisha wenyeji kwenye uwanja wao wa nyumbani hata hivyo mashambulizi hayo yaliiishia kwa kosa kosa, hadi timu inatoka uwanjani wananchi wa Musoma walishindwa kuvunga na badala yake wakajikuta wakitoa mikono ya pongezi kwa mtanange mtamu ulioonyeshwa na Kimondo Sc.
Katika kudhihirisha nia ya kupata mkoa mpya wa Songwe, Wilaya ya Mbozi kupitia wadau wake imeendelea kusukuma mbele ajenda ya michezo ambapo miongoni mwa wadau FULL DOSE ambaye amejitokeza mbele kuidhamini timu hiyo anaeleza kuwa tutaingia mkoa mpya tukiwa na timu mpya ya ligi kuu!!
 
 
Add caption