Jul 10, 2013

AGHA KHAN YAJITOSA KUOKOA UHAI WA AKINA MAMA NA WATOTO


Na Anjela Kivalala DSJ

Aga khan foundation wakishirikiana na serikali wapo mbioni kutekeleza mradi wa tuunganishe mikono pamoja unaolenga  kuboresha afya ya mama mjamzito na watoto nchini.

Aidha mradi huo unalenga  kuboresha mfumo wa rufaa kwa wagonjwa,kujenga uwezo na huduma za afya kwa mama mjawazito na watoto

 Kulingana na taarifa iliyotolewa na mfuko huo, Mradi huo pia unakusudia kuboresha  kiwango cha upatikanaji wa huduma ya afya kwa mama mjamzito na watoto, kuongeza kiwango cha matumizi ya huduma ya afya .

Kaulimbiu ya mradi huo wa tuunganishe mikono pamoja  inatafsiriwa kuwa  ‘’hakuna mwanamke ambaye atafariki wakati wa  kujifungua na hakuna sababu yoyote ya  mtoto kufariki kwa magonjwa yanayo zuilika’’. Inafafanua sehemu ya taarifa hiyo

Mpango wa mradi huo wa tuunganishe mikono  pamoja utatekelezwa katika  mikoa mitano  ya  Mwanza Dodoma Iringa Mbeya  na morogoro ili kuboresha afya ya mama mjamzito na watoto.

 Kulingana na taarifa iliyotolewa na  Aga khan health services, utekelezaji wa mradi huo  utafanyika katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia Juni 2013 kwa mikoa mitano nchini Mbeya ikiwa miongoni mwake na wilaya za Mbozi, Kyela na Mbeya zikihusika kikamilifu.

Mradi huo  unafadhiliwa na  shirika la maendeleo la Canada -CIDA  ambapo utekelezaji wake utashirikisha mashirika mengine yakiwemo  AKHST, AKU  na wadau wengine katika jamii huku wizara ya afya na ustawi wa jamii pamoja na Aga Khan Foundation wakiwa wasimamizi wa kuu wa program hiyo.