Jul 9, 2013

MAJI YAWA KERO TUNDUMA



Na Anjela Kivavala DSJ
Wakazi wa mji  wa Tunduma wamelalamika kutokana na huduma ya maji safi na salaama kuwa kero kubwa kwao.

Maji yamekuwa kero kwa wakazi wa halmashauri ya mji wa tunduma na kero hiyo ina weza kusababisha magonjwa ya mlipuko ikiwemo homa za matumbo na kuhara  kwa wakazi

 Tatizo la kukosekana kwa maji katika mji huo  limekuwa likiongezeka kila siku kutokana naongezeko la watu katika mji huo.

Wakazi wa mji huo wamekuwa wakinunua maji ya kisima kwa bei ya kuanzia shilingi mia mbili hadi mia tano kwa lita ishilini.
 hayo yamesemwa na mkazi wa mji  wa tunduma  bwana Mwafungo wakati akiiomba selikari iwasaidie kutatua tatizo hili la maji  lililo ukumba  mji huo

Mji huo ukiwa na jumla ya visima vipatavyo vinne kati ya visima hivyo ni visima viwili tu vinavyo toa vikiwa havikidhi mahitaji ya wakazi wa mji mzima tatizo hilo linaendelea kuongezeka kufuatia wakazi hao wakijenga katika vyanzo vya maji. 

Tatizo hilo limekuwa likiongezeka siku baada ya siku kutokana na ungezako la watu na makazi  atika mji huo.