Jul 13, 2013

VIFO VYA AKINA MAMA WAJAWAZITO VYAENDELEA KUIANDAMA TANZANIA


Na Anjela Kivavala DSJ

Kila saa mwana mke mmoja amekuwa akifariki dunia kutokana na  matatizo yaujauzito au wakati wa kujifungua imefahamika

Zaidi ya watoto 460 wamekuwa wakipoteza maisha  kila siku 2007 hadi 2008 idadi ya hiyo imepungua hadi  zaidi ya watoto 445 zaidi ya 140 kati yao  walikuwa na umri  chini ya mwezi mmoja  kwa mujibu wa takwimu  zilizo tolewa  wizara ya afya

 Kulingana  na takwimu zilizotolewa na  wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto  hivyo basi kuwekeza katika  huduma ya afya kutaweza kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto

 Ili kupunguza vifo vya mama na mtoto  ni muhimu kuboresha  zahanati na hospitali  hasa vijiji hili kupunguza vifo vya wanawake na watoto vinavyo tokea  nyumbani ambapo  kunakuwa hakuna vifaa vya  kujifungulia

Kupanua uwekezaji katika  huduma zisizo ghali ambazo hunusuru maisha ya mwanamke na mtoto  ikiwa ni pamoja na kutoa  vyandarua  vilivyo wekwa dawa kwa kila familia  hivyo kutapunguza vifo vitokana vyo na malaria

Kuwaelimisha wazazi wote namna ya kuyatibu magonjwa yanayo ua kama vile kuharisha na kutoa chanjo kwa watoto ili kuwa kinga na magonjwa yanayo zuhilika

Hayo yaliandikwa katika ajenda za watoto kila mama lazima awe na fursa ya kujifungua kwa kuhudumiwa na mkunga wa afya hili kuokoa maisha ya mama na mtoto.