Oct 31, 2013

DC MBOZI AKIRI USHIRIKINA KUILEMEA MBOZI, AOMBA MADIWANI WAKAKEMEE



Baraza la Madiwani la Wilaya ya Mbozi  limeombwa kushiriki katika kukemea matukio ya mauaji yaliyoanza kuibuka ambapo kwa mwezi  September peke yake kumekuwa na matukio  matano.

Akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani la wilaya hiyo Mkuu wa wilaya Mbozi Dr Michael Kadeghe amesema hali hiyo inakwamisha jitihada za kuvutia kwenye fulsa mbalimbali zilizopo kwa kujenga hofu kwa wageni

Amesema pamoja na matukio ya mauaji, pia matukio ya ushirikina katka kipindi hicho hicho yameripotiwa matukio saba

Akifafanua alisema katika kijiji cha Itaka mmoja wa watuhumiwa wa ushirikina alipohijiwa kama anajihusisha na mambo hayo alikiri kuyafanya kwa kutumia “majini”

Inaelezwa na  mkuu huyo wa wilaya kuwa katika kujaribu kupata uhakika wa anachokifanya bwana huyo, alimtaka washindane naye ambapo jamaa alianza kupandisha maruhani yake ili amfanyie uchawi Dc  hali ambayo bwana Kadeghe alilazimika kumzima kwa kumzuia asiendelee

Huku madiwani wakicheka kwenye kikao hicho, Dc alisema kama huyu jamaa alikuwa tayari kufanya ushirikina mbele ya kamati ya ulinzi na usalama unadhani wananchi wa kawaida huko chini hali inakuwaje?

Alisema katika hatua nyingine kumekuwepo matukio ya mara kwa mara ya wanavijiji kuwafukuza watu wanaotuhumiwa kufanya ushrikina vijijini na kwamba katika matukio ya hivi karibuni walimwokoa mwanamke mmoja aliyekuwa aliyetuhumiwa katika kata ya Nambinzo.

Alisema kasi ya wanavijiji kuwahamisha watuhumiwa wa vitendo vya kishirikina wilayani humo vinaashiria kuwa matukio ya imani hizo yamewachosha na yanaweza kusababisha kutoweka kwa amani kwenye jamii.


Alisema yeye hana uwezo wa kuhamisha watu kwenye vijiji na mamlaka hayo anayo mheshimiwa rais pekee hivyo kumekuwa na ugumu kufanya maamuzi ya namna hiyo licha ya viashiria vya ushirikina katika jamii kuoneka.