Oct 23, 2013

KAMATI YA BUNGE YAOMBA IKAJIFUNZE KUTENGENEZA MVUA MALAYSIA

Na Danny Tweve Mbozi

Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Mbunge wa jimbo la Mwanakwerekwe Mh Haji Jumaa Sereweji amesema kuna haja kwa wizara ya Kilimo kuipeleka kamati hiyo kwenda kujifunza namna mvua  za kutengenezwa zinavyoweza kuleta ufanisi

Mbunge huyo akichangia hoja iliyoanzishwa na Mbunge wa Rungwe magharibi Profesa David Mwakyusa kuwa serikali ianze kubadilisha mfumo wa kusaidia maeneo yenye njaa kwa kupeleka chakula na badala yake fedha zinazotengwa kwaajili ya kununua chakula cha akiba zielekezwe kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa maeneo yenye ukame.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwenge wilayani Mbozi bwana Mwaipwisi akitoa malalamiko juu ya uharibifu wa barabara unaofanywa na magari yanayopeleka shehena ya mahindi kwenye maghala hayo pasipo kutozwa fedha za matengenezo ya barabara hizo na kuliacha jukumu hilo kwa mamlaka ya mji wa Vwawa

Mtendaji Mkuu wa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula Bw. Charles Walwa akizungumza na wakulima na mawakala waliouza mahindi yao kwenye kituo cha Vwawa wilayani Mbozi

Miongoni mwa zana za kuchambua uchafu wa mahindi yanayofikishwa kituoni hapo na wakulima kwa njia za udanganyifu kwa kuweka takataka kwenye magunia yao 

shenena ya mahindi ambayo inasubiri kusafirishwa kwenda Makambako na jijini Dar es salaam kutokana na maghala kutotoshereza wingi za mahindi yaliyopo

 Mtendaji wa NFRA BW. CHARLES WALWA akijibu hoja za kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji liyofanya ziara kwenye maghala ya Vwawa wilayani Mbozi ambako shehena kubwa imeanza kusafirishwa kupelekwa jijiji
 sehemu ya shehena ya mahindi yaliyopo kwenye ghala la Vwawa


 Wabunge wakihoji ubora wa magunia yanayotumika katika uhifadhi wa nafaka kwenye ghala la NFRA Vwawa Mbozi
 Mbunge wa Sikonge Mh Said Nkumba akizungumza na wafanyabiashara, mawakala na wakulima waliouza mahindi yao kwa wakala wa hifadhi ya chakula ya Taifa NFRA katka kituo cha Vwawa ambapo wanalalamikia kucheleweshewa malipo yao
Ujumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na mtendaji mkuu wa wakala  NFRA

Mh Sereweji alisema yeye kwa mtazamo wake Tanzania ya sasa haipaswi kuendelea kusubiria umwagiliaji wa kutegemea mvua za mwenyezi mungu ambazo zinaathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi, na kwamba ubunifu na matumizi ya teknolojia za umwagiliaji zaidi zikiwemo mvua za kutengeneza
Ningeshauri kamati hii ipelekwe kuleee wapi kule malasia ili ikajifunze na kuona ufanisi wa mvua hizo ili teknolojia hiyo iletwe nchini na kutumika kwaajili ya kuongeza uhakika wa chakula hasa kwa maeneo yenye ukame.
Akizungumza kwenye ziara yao ya kushtukiza walioifanya kwenye ghala la kusafirishia nafaka la Wakala wa hifadhi ya Taifa ya Chakula NFRA  lililopo eneo la Vwawa wilayani Mbozi , Mbunge wa Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa alisema kuna baadhi ya maeneo nchini yamejipa hati miliki ya misaada ya chakula kila msimu licha ya maeneo hayo kuwa na fulsa zingine za uzalishaji.
Profesa Mwakyusa alisema kuna umuhimu kwa maeneo hayo kuhamasishwa kuanzishwa mifumo ya umwagiliaji ambayo itawezesha  kufanya umwagiliaji pale mvua za zinaposimama na kwamba fedha zinazotengwa kununua nafaka zielekezwe kwenye miradi hiyo ya umwagiliaji.
Katika taarifa yake Mtendaji Mkuu wa wakala wa hifadhi ya Chakula nchini NFRA Bwana Charles Walwa alisema wakala yake imepokea kiasi cha shilingi Bilion 70 kwa mwaka wa fedha 2013/2014 kati ya Bilion 100 ilizozitarajia kwaaajili ya kulipa kwa wakulima na mawakala kutokana na ununuzi wa nafaka
Alisema wakala yake ina imani kuwa deni la bilioni 30.2 litalipwa mapema ili kuwezesha wakulima kuendelea na hatua za maandalizi ya msimu ulioanza wa kilimo na kwamba wakulima na mawakala wawe wavumilivu kwa muda mfupi huu ambao maalipo hayo yanaandaliwa hazina.
Mtendaji huyo amesema katika hatua za kuipunguzia gharama za uendeshaji, wakala hiyo inafanya mazungumzo na makampuni ya hapa nchini kuanza kutengeneza mifuko ya visalfeti kwaaajili ya kuhifadhi nafaka badala ya kutumia magunia ambayo bei zake zimekuwa zikipanda msimu hadi msimu.
Alisema wakala imekuwa ikitumia kiasi cha shilingi Bilion 5 kwa kila msimu kwaajili ya kununua magunia ya katani kwa ajili ya kuhifadhi nafaka ambayo yamekuwa yakiharibika katika kipindi kifupi tofauti na teknolojia ya visalfet ambayo inatumiwa na nchi jirani kama Zambia ambayo imeonekana inapunguza gharama zaidi ya nusu ya ile wanayotumia sasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayosimamia Kilimo, Mifugo na Maji Mh SAID MKUMBA  ameelezea kuridhishwa na jitihada za wakala hiyo katika kujipanga kwaajili ya kujitegemea
Alisema hatua za sasa za kuanza kujenga na kupanua maghala ni hatua muhimu ya kuonyesha uwezo wake katika ukusanyaji wa mazao na kulipa kwa bei nzuri kwa wakulima.
Alisema kiwango cha shilingi 500 kwa kilo kiliweza kuvutia wakulima wengi kuuza mazao yao kwa NFRA  hivyo hatua iliyobakia ni kuendelea kujenga imani hiyo kwa wakulima kwa kuhakikisha wanalipwa kwa wakati ili waendelee kushiriki uzalishaji kwa tija.
Kamati hiyo ya Bunge ilizungumza pia na mawalaka na wakulima ambao wanaidai NFRA ambao miongoni mwao walionyesha kuchoshwa na ahadi za malipo yaliyocheleweshwa yanayofikia Bilion 30.2kwa nchi nzima huku kiasi kikubwa kikiwa ni wakulima wa mikoa ya Mbeya na Rukwa.

Mwisho