Oct 31, 2013

PROFESA MHONGO AKWEPA KUZUNGUMZIA SUALA LA KUVUJA MAFUTA KWENYE VISIMA VYA MAJI MLOWO

na Mwandishi wa Indaba Africa
Waziri wa nishati na Madini Mh Profesa Sospeter Mhongo jana ameruka viunzi sakata  la kuvuja kwa mafuta ya diesel kwenye visima vya maji katika mji wa Mlowo na kudai kuwa halihusiani na wizara yake
Akizungumza jana  wakati akijibu swali la mmoja wa Madiwani aliyetaka kujua serikali inafanya nini wakati wananchi wa Mlowo wakiwa afya zao zikiwa hatarini kutokana na kuchota mafuta badala ya maji kwenye visima vya mji huo.
Suala hilo liliwasilishwa na diwani wa Myovizi Mh Cosmas Nzowa ambaye alihoji kama waziri anayeshughulikia masuala ya nishati ambapo mafuta ya diseli ni sehemu ya mamlaka ya waziri huyo ambapo waziri alikuwa akimkatiza katiza wakati diwani huyo akiuliza
“masuala ya mafuta ya diseli ninahusikaje mimi? Waulize NEMC hilo ni suala lao “ alisikika waziri Mlongo kabla ya diwani huyo kufafanua
Diwani huyo alisisitiza suala la Mafuta ni sehemu ya wizara ya Mlongo labda kama imebadilika na ndipo Mlongo aliporuhusu aendelee kuuliza swali lake, “ haya endelea bwana”  uliza tu
Hata hivyo pamoja na swali hilo kuulizwa  kwa lengo la kutaka majibu yam h waziri, inaonekana waziri alilikwepa katika kutoa  majibu pale ambapo alizungumzia zaidi masuala ya Umeme  na jitihada zinazofanyika mkoani Mbeya na pia kwa wilaya ya mbozi  lakini kwenye mafuta ya Mlowo alikauka!
Kwa ujumla wakazi wa mji wa Mlowo wamekuwa wakilalamikia hali mbaya ya maji ya visima vyao kunakotokana na mwingiliano wa mafuta ya diseli yanayohofiwa kuvuja kutoka kwenye bomba la Mafuta la TAZAMA ama kutoka kwenye moja ya visima vya mafuta vilivyopo kwenye vituo vya Mlowo.
Diwani wa Myovizi Cosmas Nzowa akisalimiana na Mh Profesa Mhongo alipofanya ziara yake katika wilaya ya Mbozi kwa lengo la kukagua miradi inayotekelezwa na  Wakala wa Umeme vijiji  REA jana 
Katika majumuisho yake kwenye kikao chake kilichofanyika ukumbi wa mkuu wa wilaya Mbozi, Waziri Mlongo alielekeza   wananchi kuwa  na nia njema ya kugawa maendeleo sawia katika meneo yote ya nchi badala ya kuwa na uroho wa kila fulsa kuwa kwenye maeneo yao.
Hali hiyo ilitokana  na kila diwani aliyesimama kwenye kikao hicho kuvutia umeme kwenye maeneo yake kuwa haujapitia, na ndipo alipomwinua mbunge wa  Mpanda –Katavi Saidi Kessy na kumuuliza, hivi wewe Kessy kule kwako umepewa kiasi gani na REA?
Mh Kessy alijibu Bilion 10. Mheshimiwa  waziri na Mkoa wa RUkwa umepewa Bilion 30!
Ndipo alipodakia hapo waziri na kueleza” Nyinyi Mbozi kama wilaya mmepewa Bilion 22.57 wakati wenzenu Rukwa kama mkoa wamepewa Bilion 30 hamuoni kuwa mmepata kiasi kikubwa sana? Sasa tukielekeza kila kitu kwenye wilaya yenu jamani tuwe na ulinganifu.