Oct 30, 2013

PROFESA SOSPETER MHONGO AWAPIGA DONGO MADIWANI, MSIPENDE SAFARI MNO!!


 PROFESA MHONGO ALIPOWASILI MBOZI AKISALIMIANA NA MKUU WA WILAYA YA MBOZI DR MICHAEL KADEGHE, NYUMA YAKE NI MBUNGE WA KATAVI MHE. SAID KESSYNA MWENYE SHATI LA KIJANI NI MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA MBOZI ERICK MINGA
 BAADHI YA WATENDAJI WA WILAYA YA MBOZI PAMOJA NA UJUMBE WA TANESCO WAKIFUATILIA KIKAO HICHO



 KAIMU MKURUGENZI MBOZI DR CHARLES MKOMBACHEPA na MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA MH CHARLES MINGA AMBAKISYE
Mh Profesa Mhongo akizungumzia hali ya huduma za umeme na nafasi za halmashuri  za wilaya katika kuchangia miradi ya UMEME nchini
 BAADHI YA WAKUU WA IDARA NA VITENGO HALMASHAURI YA WILAYA NA SERIKALI KUU WILAYANI MBOZI WAKIFUATILIA MAJADILIANO
 PROFESA MHONGO AKIZUNGUMZA NA WATAALAM HAO PAMOJA NA MADIWANI
AKISALIMIANA NA BAADHI YAWATENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI

NA DANNY TWEVE INDABAAFRICA MBOZI 

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo amewataka madiwani nchini kuachana na mitazamo ya kizamani kuwa kila suala linalohusiana na maendeleo ni lazima lielekezwe kwenye serikali kuu wakati wao wanakalia rasrimali zinazoweza kutatua kero hizo.

Akizungumza baada ya kupokea maswali mbalimbali kutoka kwa madiwani wa wilihohudhulia katika mapokezi yake wilayani Mbozi, Mhongo amesema ni vyema sasa halmashauri zikaanza kutenga fedha kwaajili ya kufadhiri miradi ya umeme kama inavyofanyika kwenye miradi mingine

Alisema hali hiyo itasaidia kusukuma mbele jitihada za kujiletea maendeleo na hasa kwa kuzingatia kuwa REA pia imejielekeza katika utekelezaji wa miradi ya umeme wa jua kwaajili ya maeneo maalum kama shule.

Profesa Mhongo alisema ni vyema Madiwani kuachana na ziara na safari zisizo na tija kwa halmashauri zao na kuendelea kutumia vibaya rasrimali za taifa wakati mahitaji ya wananchi ni makubwa kwenye masuala yanayohusiana na maendeleo hususani Umeme na huduma zingine

Alitolea mfano miradi ya umeme wa jua kwenye shule za sekondari zenye madarasa 8 mitambo yake inaghalimu kiasi cha shilingi millioni nne ambazo halmashauri za wilaya zinaweza kutenga kwenye mapato yake na kuwaita REA ili wawezeshe ufungaji wa umeme huo.

Aidha akifafanua hali ya upatikanaji wa umeme nchini Profesa Mhongo amesema kwa sasa  hali ya upatikanaji umeme vijijini ni asilimia 7 na lengo ni kufikia asilimia 20 ifikapo 2015.

Kwa upande wa upatikanaji wa umeme kwa ujumla nchini alisema asilimia 20 ya watanzania wanapata umeme na lengo ni kufikia asilimia 30 ifikapo 2015 ingawa msukumo mkubwa unaelekezwa vijijini

Akitoa takwimu za jumla Meneja Msaidizi wa ufundi wa REA bwana GISSIMA NYAMBO –HANGA alisema kwa wilaya ya Mbozi na Momba REA imetenga shilingi Bilion 22 kuwezesha  umeme  katika vijiji vya wilaya ya Mbozi
Alitaja baadhi ya maeneo yaliyopo kwenye mpango huo ni pamoja na Kamsamba, Hasamba, Hatelele, Isansa, Msanyila, Msia, Nanyala, Senjele, Mbimba, Nkanga, Oldvwawa, Itaka, Itepula, Ndalambo, Msangano, Hezya na Ivwanga

Alisema wateja wa awali 2700 wataunganishwa na mfumo huo wa umeme na kwamba hatua za kumpata mkandarasi zipo mbioni na kwamba utekelezaji wa miradi hiyo utaanza November 2013.