Oct 21, 2013

WADAU WA ZAO LA MPUNGA WALALAMIKIA UINGIZAJI MCHELE KUTOKA NJE

Akina mama wanaouza mchele kwenye eneo la Soko la Sumbawanga wakiwaeleza maofisa kutoka Shirika la Maendeleo la Uholanzi SNV changamoto ya soko la mchele wa ndani kushindwa kupenya baada ya uamuzi wa serikali kuingiza mchele kutoka nje ambapo wanunuzi wa awali ambao ni kutoka mkoani Dar es salaam sasa hawafiki Sumbawanga kufuata mchele huo

Mama huyu aliamua kusimama na kutoa ufafanuzi namna wanavyokwamishwa na hali ya sasa ya wanunuzi kutofika mkoani Rukwa kufuata mchele huo kutokana na mchele kutoka nje kuuzwa bei ndogo ikilinganisha na ule unaozalishwa na wakulima mkoani humo

Wadau wa zao la Mpunga mkoani Rukwa wakitoa maoni yao juu ya mnyororo wa thamani  wa zao hilo na kuweka mikakati ya kujenga mtandao wa wazalishaji wa mpunga mkoani Rukwa 

miongoni mwa watoa maamuzi kwenye ngazi ya halmashauri ambao ni madiwani walishiriki katika mjadala huo ambao unalenga kuweka mikakati ya kulifanya zao la Mpunga kuwa eneo muhimu la kiuchumi linalochangia pato la wananchi wa mkoa wa Rukwa  kama yalivyo mazao mengine ya biashara ambayo yameundiwa bodi zake

Mratibu wa MVIWATA mkoa wa Rukwa  akifutilia michango ya wadau wa zao la Mpunga kwenye mkutano huo ambao ulihusisha wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya fedha, makampuni ya mbegu na vifaa vya kilimo mkoani Rukwa

Afisa kutoka Shirika la Maendeleo la Uholanzi SNV Bw Joel Mwakitalu akizungumzia nafasi ya wakulima katika kuchukua hatua za kujenga mtandao utakaowawezesha kuwa na mawasiliano ya pamoja baina yao,vyombo vya fedha na wasambazaji mbegu na huduma zingine ili kuongeza uzalishaji wenye tija na kulifanya zao muhimu kiuchumi kwa vijana na jamii kwa ujumla

Afisa  Kilimo wilaya ya Sumbawanga kushoto akifuatilia michango ya wadau kwenye mkutano huo