HAPA ilikuwa Sept 15 ambapo mpaka baina ya Kongo na Rwanda ulifungwa baada ya kutuhumiana na hiii inafuatia Rwanda kudai Kongo imeua raia wake kwa kupiga kombora wakati ambapo kongo ilidai ni waaasi wa M23 walifanya hivyo kuongeza chumvi kwenye vita hiyo ili Rwanda aikasirikie kongo
Hapa kikosi ch jeshi la Kongo kikisonga mbele baada ya kuanza kukomboa maeneo muhimu ya ngome ya waasi wa M23
Baada ya mziki kuzidi jana usiku, M 23 Waliamua kuanza kuteketeza baadhi ya zana zilizokuwa zikiwasaidia, hii inaitwa bora wote tukose! hasa inapoonekana kuwa huna matumaini tena ya kwenda mbele zzaidi ya kutafuta mahala pa kujificha!!!
Hii ndiyo iliyokuwa kambi ya M 23 Makao makuu yao, lakini baada ya kuvurumishwa wakaamua kuiteketeza kabisa jana na leo kabla ya kutangaza kisanii ati wameacha vita ili wafanye mazungumzo ya amani!
Mateka na vijana waliojisalimisha kutoka kikundi cha M 23
Zana zilizoharibiwa na kundi la M 23 baada ya maji kuwafika shingoni, hapa ni moja ya makambi yao katka eneo la Chanzo ambako ndiko makao makuu ya M23
Upepo ulivyosoma vibaya waliamua kutelekeza mashine kama hizi za kivita na kutimua mbio kusikojulikana
Kwaheri ya kuonana kifaa chetu, siye tunakwenda " ndivyo zana hii inavyoonekana kuachwa
Hapa ndipo jamaa wa M23 walipojihifadhi kwa siku tatu za hivi karibuni lakini baada ya chai ya kuanzia jana jioni, usiku na hatimaye asubuhi ya leo wametangaza wenyewe kutupa chini mikoba
Hapa ni kambi yao iliyoharibiwa baada ya kukumbana na wakati mgumu wa jana na leo usiku!
Kiongozi wao amekuja na maelezo haya kwa kifaransa nitayafafanua
nnonce de fin de rébellion
Annonce de fin de rébellion
La Direction du Mouvement du 23 Mars annonce à l'opinion nationale et internationale qu'elle a décidé à dater de ce jour de mettre un terme à sa rébellion et de poursuivre, par des moyens purement politiques, la recherche des solutions aux causes profondes qui ont présidé à sa création.
A cet effet, le Chef d'Etat-major Général ainsi que tous les commandants des grandes unités de l'Armée Révolutionnaire Congolaise sont priés de préparer les hommes des troupes au processus de désarmement, démobilisation et réinsertion sociale dont les modalités sont à convenir avec le Gouvernement de la République Démocratique du Congo.
Fait à Kampala, le 05 Novembre 2013
Le Président du Mouvement du 23 Mars
Bertrand BISIMWA
Kwa kiswahili cha haraka haraka ni kwamba
Mwisho wa Uasi
Mwisho wa Uasi
Kurugenzi ya Movement on March 23 ama kwa kifupi M23 inalitangazia taifa na jumuiya ya kimataifa kuwa kuanzia tarehe ya siku ya leo kusitisha uasi wake, na sasa mazungumzo ya kisiasa yatachukua nafasi katika kutafuta suluhu na kutafuta chanzo kilichotuleteleza kwenye hali hii ya mapigano
Kwa mwisho huu Amiri jeshi Mkuu na wakuu wa kamandi zake na vikosi vyake (m23) wanatakiwa kuvunja vikosi vyote, kuweka siraha chini na kusitisha mapigano tena ili kuunganisha nguvu na jamii ya watu wa kongo wakati huu tuweze kutekeleza yale tuliyokubaliana na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
Limetolewa hapa Kampala ,November 5, 2013
Rais wa Movement of March 23
Bertrand Bisimwa