Mar 23, 2014

JAMVI LA LIGI DARAJA LA KWANZA LAKUNJWA HUKU KIMONDO IKIRUKA KIMANGA KUSHUKA DARAJA

 
Na Danny Tweve
 
Timu ya Kimondo supersport club ya Mbozi mkoani Mbeya, imemaliza mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza Tanzania kwa kuikamua Mlale JKT ya Songea bao 1-0 katika mchezo mkali uliochezwa uwanja wa CCM Vwawa.
 
Ulikuwa mchezo wa kasi na kusisimua tangu kuanza kwake, lakini kadiri dakika zilivyoyeya ndivyo mhemuko wa mashabiki kutaka goli la kuwahakikishia Kimondo kuendelea kucheza ligi daraja la kwanza ukizidi
 
Mchezo huo ulikuwa muhimu kwa Kimondo ili kujiweka katika mazingira ya kutoshuka daraja kutokana na Kimondo kuwa moja ya timu katika kundi hilo zilizokuwa na pointi 14 huku pia timu ya Mkamba ambayo ilikuwa mkiani ikiwa na pointi 13
 
Matokeo ya jana yanaifanya Kimondo ambayo ilikuwa kundi B kujipanga upya baada ya kutoa fulsa kwa timu ya Polisi Morogoro kuondoka ikiwa na ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Vwawa licha ya ukweli kwamba tayari Polisi moro ilikuwa imeshajitangazia kupanda daraja katika mchezo wake na Maji Maji Morogoro hivyo kufikisha pointi 28 ambazo zisingefikiwa na timu yoyote

Licha ya jitihada za wazi za kuvuruga mchezo huo zilizofanywa na MLALE JKT ikiwa ni pamoja na kocha wao kuamua kuzunguka uwanja mzima kinyume na taratibu za mchezo huku akikoromeana mara kwa mara na waamuzi, mchezo ulimalizika kwa Kimondo kunyanyuka ikiwa na ushindi wa bao 1-0