Hatimaye Mbwana Ally Sammatta ameiwakilisha vyema Tanzania baada ya kushinda miongoni mwa wachezaji wazawa wa Afrika kama mchezaji bora wa Mwaka anayechezea ligi za ndani ya Afrika
Samatta anaungana na Mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Gabon kuwa vinara wa CAF kama wachezaji bora wa mwaka 2015 kwa mara ya kwanza.
Samatta anakuwa mchezaji wa kwanza ukanda wa Afrika Mashariki kutwaa tuzo hiyo akiwa mchezaji bora anayeshiriki ligi za ndani barani Afrika
Mbwana Samatta amewafunika wenzake akiwemo mchezaji mwenzie wa Tp Mazembe na kipa wa DRC CONGO Robert Muteba Kidiaba ambaye aliinuka na pointi 88, na kufuatiliwa na mchezaji kutoka Lgeria Baghdad Bouneydjah aliyepata pointi 63
Wakati utamu huo ukimjia Samatta na taifa lake Tanzania, Majonzi yamehamia kwa wachezaji wakongwe akiwemo Yaya Toure kutoka Ivorycost na Ayew Andre wa Ghana ambao wamenyanyasika mbele ya mchezaji kinda wa miaka 26 Aubameyang aliyezoa pointi 143 zikiwa saba zaidi ya alizopata Toure huku Ayew akipata 112
chanzo vanguard