Timu ya Umoja wa wanafunzi wa Sekondari -Mkoa wa Songwe, imo kwenye hatua za mwisho kwenda kushiriki mashindano ya Taifa yanayokusudiwa kufanyika Mkoani Mwanza. Timu hiyo imeundwa rasmi na orodha ya wachezaji kusomwa mbele ya afisa elimu Mkoa wa Songwe JUMA MHINA juzi katika uwanja waa shule ya sekondari ya Vwawa.
Timu hiyo yenye wachezaji 120 itawakilisha mkoa wa Songwe katika michezo ya Mpira wa Miguu kwa wanaume, Mpira wa Pete, Riadha, Mpira wa mikono, Mpira wa Kikapu na michezo ya ndani.Mkoa wa Songwe ndiyo bingwa wa taifa ka mwaka uliopita ambapo iliweza kuwadungua Unguja kwenye mpira wa Miguu katika fainali.