Adverts

Apr 30, 2009

DARAJA LA MNING'INIZO

Hii picha nimedowea kwa mdau wangu maisha ni vita.blogspot.com.
Hili ni ja ya madaraja yaliyojengwa na Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF wilayani Mbozi, ila daraja kama hili ukiwa chicha unaweza kujiachia, manake linanesa eeeee, hadi unamwaga pombe zote kichwani.
Hongera Tasaf Mbozi kwa kuwasogezea wananchi huduma manake walikuwa wanaogolea kwenye mto kwenda upande wa pili, sasa wanafunzi inakuwaje pale wanahitaji kwenda shuleni?