Adverts

May 28, 2011

AJALI YA SUMRY TAARIFA RASMI WALIOFARIKI SASA NI 15

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya ADVOCATE NYOMBI amesema idadi ya waliokufa katika ajali ya Sumry iliyotokea jana majira ya saa 4.45 Usiku ni watu 15. Akizungumzia ajali hiyo kamanda Nyombi amesema gari hilo limepinduka baada ya kupasuka kwa gurudumu la Mbele na kwamba sehemu kubwa ya majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya misheni ya Ilembula na Chimala.
Amesema gari hilo likitokea Arusha lilikuwa katika mwendo kasi na baada ya kupasuka gurudumu la mbele dereva alishindwa kulimudu hatua ambayo lilikwenda pembeni na kupinduka hatimaye kukatika eneo la juu kuanzia kwenye vioo na kusababisha vifo15 na majeruhi 20.
Dereva wa gari hilo ni miongoni mwa waliofariki papo hapo.

Hili ni tukio la pili katika kipndi cha miezi minne ambapo January 13 basi jingine la Sumry lililokuwa likisafiri kati ya Dar na Mbeya katika eneo la Mikumi  liligongana na roli aina ya Fuso katika eneo la Masimba -Mikumi na  na kuua watu 8 na wengine 20 kujeruhiwa.
Waliokufa katika ajali ya jana bado majina yao hayajawekwa hewani na taarifa zaidi zitawajia baada ya muda mfupi kwani ripota wetu yupo eneo la Tukio kwa sasa.
endelea kuwa nasi www.dtwevetz.blogspot.com