Adverts

Jun 28, 2011

ALJAZEERA RESTAURANT KULA DAKIKA 10!!!!

Hapo ndipo Aljazeera restaurant ambapo abiria anayetokea Dar ama Mbeya lazima apapitie, sasa cha kufurahisha ni matangazo ya ABIRIA KULA DAKIKA KUMI!!!  hivi wataalamu tuambieni biunadamu anatakiwa achukue dakika ngapi wakati wa kula?

Bidhaa zilizopo zinazingatia mahitaji ya makundi mbalimbali wapo wanaotaka vitu vigumu vigumu na wale wa vitu laini!!!!

Hapa mahudhulio zaidi ni akina dada !!!Chipsi kuku!!!

Unakokwenda lazima uende na zawadi, pitia hapa nunua halafu unapokelewa kwa heshima siyo mikono mitupu!!!

Twanga tuuuuu!!! ongea mpaka basi, Aljazeera imeunganishwa kwa mawasiliano bila kujali mazingira yake kuwa porini!