Adverts

Jul 23, 2011

BRECKINGNEWS>BAADA YA HALI YA HEWA KUCHAFUKA TUNDUMA, OMARY NUNDU ATOKEA MCHANA HUU



Taarifa zilizoufikia mtandao wa Indaba zinasema, waziri wa uchukuzi Omary Nundu atazungumza mchana huu na madereva wa magari yanayosafiri kati ya Tanzania na nchi zingine kupeleka na kuleta mzigo maarufu kama Transit.
Mkutano huo ni matokeo ya kugomewa kwa jitiohada zote zilizofanywa na viongozi wa mkoa wa Mbeya ambapo mkuu wa mkoa wa Mbeya John Mwakipesile jana alimtuma mkuu wa wilaya kupeleka ujumbe wa kuwataka wasitishe mgomo huo wakati mambo yao yakishughulikiwa, lakini wakati mkuu huyo wa wilaya akisoma barua hiyo alipofikia mwisho akataja imesainiwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya John MWAKIPESILE ghafla wakalipuka kuzoea,

Awali walikuwa wakipiga makofi kwa kila kipengere kilichosomwa, lakini ilipofika hatua ya kusoma aliyeandika waraka huo basi hali ikawa siyo, jambo linaloashiria kuwa walihisi hizo zilikuwa ni porojo za kuwatuliza na si ujumbe kutoka kwenye mamlaka za juu kama walivyotaka.\
Omary Nundu amelazimika kufika leo hii baada ya gari moja lililokuwa likiendeshwa na mtanzania mwenye asili ya somalia kuzuiwa na madereva wenzake likiwa barabarani na kisha wakachomoa funguo na kutokomea nazo, hivyo kuzuia shughuli za barabra kuu ya Tunduma -Mbeya.
Imeelezwa kuwa gari hilo linatumia passwords ama mzingo katika kuliwasha ambapo pia ni lazima funguo iwe halisi ambapo vibonyezeo vyote vipo kwenye funguo hali ambayo ililazimu polisi kuwa wapole kwani walishaanza kubutua mabomu.

Kilicjhotufikisha hapo ni matokeo ya serikali kuchukulia juu juu mgogoro huo ambapo ilionyesha kuto kuupa uzito unaostahili katika kushughulikia zmalalamiko waliyoyatoa madereva yakihusisha haki zao pamoja na baadhi ya kero ambazo tayari zimeanza kupatiwa ufumbuzi.
Madereva hao walianzisha changamoto hiyo tangu  July 17 baada ya kuandika barua kwenda kwa waziri mkuu lakini ikakosa majibu kwa kipindi chote hatua ambayo wakaamua kuchukua maamuzi lakini wakionyana wenyewe kutokujihusisha na uharibifu wa mali.
Hata hivyo taarifa zilizozagaa jana zilianza kuonyesha hofu kubwa baada ya kudaiwa baadhi ya madereva hao wametegesha petroli kulipua magari ikiwa polisi wangetumia mabomu ama kuanzisha operesheni ya FFU, hatua hiyo iling,amuliwa na idara za Inteligensia ambapo magari ya zima moto yaliandaliwa jana kukabili hali hiyo wakati magari ya washa washa yalipokuwa yakizunguka na kutoa tahadahari jana jioni. 
Mtaendelea kuelezwa kinachoendelea kupitia blog hii