Adverts

Jan 21, 2012

Mwizi wa simu adandia maghorofa Dar na kutokomea kama Ninja

Mtuhumiwa wa wizi wa simu, akiruka kutoka juu ya ghorofa, wakati akifukuzwa na wananchi wenye hasira baada ya kukamatwa akiwa ameiba simu na kuwazidi mbinu na kuwaponyoka, kwa kudandia maghorofa moja baada ya nyingine kama Ninja, kwenye Barabara ya Uhuru, Dar es Salaam leo, kama inavyoonesha katika picha hizi.
Hapa wananchi wenye hasira wakimpa mkongoto, baada ya kumkamata
Hapa baada ya kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi baada ya kupata kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali waliomkamata
Hapa wnannchi wakiwa wamekata taamaa baada ya mwizi huyo kupita kwenye tundu hili na kuruka kutoka juu ya ghorofa na kutokomea kusikojulikana leo.