Adverts

Jan 23, 2012

RAISI KIWETE, MIZENGO PINDA WAONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI

Rais Dk. Jakaya Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Arumaru Marehemu Jeremiah Sumari katika mazishi yaliyofanyika mkoani Arusha leo huku rais Jakaya akiongoza mamia ya waombolezaji.

NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE- ARUSHA

ALIYEKUWA Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Jeremiah Sumari amezikwa jana kijijini kwake Akheri wilayani Meru Mkoani hapa na mazishi hayo kuongozwa na Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya kikwete, pamoja na waziri mkuu Bw Mizengo Pinda.

Akiongea na waombolezaji waliofika katika eneo hilo la Akheri waziri Pinda alisema kuwa viongozi mbalimbali wa Serikali wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kama alivyokuwa Bw Sumari

Bw Pinda alieleza kuwa kiongozi kama kiongozi anatakiwa kuwa na sifa ambazo zitamfanya jamii imlkumbuke mara zote na sifa hizo zinatakiwa kuwa ni miongoni mwa sifa nzuri na zenye kulijenga taifa.

“hii ni safari ya Bw Sumari lakini sote tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunaweka hazina hapa duniani, na kuwa na sifa nzuri na zenye kupendeza, kwa kuwa kifo ni msingi wa kila mwanadamu hapa duniani”aliongeza bw Pinda.

Pia aliitaka familia ya Marehemu Sumari kuhakikisha kuwa haioni mzigo kwa kuondokewa na Baba yao na badala yake wahakikishe kuwa wanaendelea kumtegemea zaidi Mungu katika mambo yao ikiwa ni pamoja na kufuata Mambo mazuri ambayo yalikuwa yanafutwa na Bw Sumari.

Katika hatua nyingine viongozi mbalimbali ambao waliongoza ibada hiyo ya Mazishi walisema kuwa kwa sasa jimbo la Arumeru Mashariki limepoteza Mbunge wake kwa maana hiyo ni lazima taratibu za kumtafuta Mbunge huyo zifanyike wakati utakapofika lakini wagombe wanatakiwa kuwa makini na kuachana na tabia ya uchakachuaji wa matokeo

Walibanisha kuwa endapo kama zoedzi la uchakachuaji wa matokeo katika jimbo hilo ni wazi kuwa watakuwa wanaweka jimbo hilo mashakani kabisa hali ambayo itachangia matatizo mbalimbali juu ya jimbo hilo.

“tunatangaza rasmi kabisa kuwa hapa hamna masuala ya kuachakachua matokeo kwa maana hiyo uchaguzi utakaokuja ni lazima matokeo yawe ya halali kwa maslahi ya jimbo hili”waliongeza wachungaji hao.

Aidha nao viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) walisema kuwa wao kama chama kupitia kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo walikuwa na ahadi nyingi dhidi ya jimbo hilo ambapo ahadi hizo zilikuwa na lengo la kusaidia jamii.

Walisema kuwa ahadi za mbunge huyo kwa jimbo hilo ziko palepale na zitatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya chama hicho kwa eneo hilo la Arumeru Mashariki ili kuweza kupambana na changamoto mbalimbali.