Sep 27, 2010

MTANZANIA HUYU ANA HAKI YA KUCHAGUA NA KUCHAGULIWA

Ni Watanzania wangapi wenye umri kama huu waliowezeshwa na kuandaliwa vyema kushiriki uchaguzi mkuu 2010? je wanajua utaratibu mzima wa kufikia kwenye chumba cha kupigia kura? wanafahamu wapi pa kuweka alama ya ndiyo kwa mgombea wanaomtaka? elimu ya mpiga kura vijijini imewafikiaje? Kapu hili lina matumaini ya kujazwa  lakini je viongozi mtamwezesha mtanzania huyu ambaye kapu lake la matumaini limekuwa wazi litapata kujaa yale anayoyakusudia kupata katika kipindi chenu cha uongozi kama mnavyotuambia kwenye ilani zenu za uchaguzi.