Sep 27, 2010

VIJIJINI NAKO KUZURI BWANA

Asikuambie mtu Kijijini nako kuzuri bwana , hebu angalia mazingira haya hayajachafuliwa na lolote, unadhani wasabato masalia walikosea kuhamishia familia zao vijijini?  sema sasa vijijini fulsa ndizo zinabanwa manake mambo ya Televisheni kama huna umeme wa uhakika huoni mpaka Padre aje ama kwenye kituo cha afya kwa mganga mkuu, sisi tumezoea kuita kwa bwana mganga  hata kama ni nesi wa kawaida!.Hapa bwana panaitwa Hospitali ya ITETE wilayani Rungwe, nilipapenda mno mahala hapa.