Sep 27, 2010

VIJIJINI TUNAPENDA MIZIKI KAMA HII

Kwa taarifa yako Shughuli za vijijini bila burudani haziendi, kwetu sisi Mbozi bila huyu jamaa shughukli yako haifanikiwi. Anaitwa Mawazo Tulyanje Mwana mziki wa asili ambaye ameimba nyimbo maarufu zinazopigwa mara kwa mara kwenye shughuli kama harusi, wimbo mmojawapo maarufu unaitwa MWINGA. huyu bwana balaa hasa katika kutunga maneno papo kwa papo nakumbuka siku moja nilikuwa mgeni rasmi mahala nikajikuta natoa kaposho kangu kote kumtuza eti amenitaja jina langu mbele ya wananchi si unajua vijijini tunavyopenda ujiko!!!!!