Jan 30, 2011

Muasi wa Rwanda afikishwa mahakamani “The Hague”

Muasi wa Rwanda afikishwa mahakamani “The Hague”: "

Callixte Mbarushimana kiongozi wa waasi wa Rwanda amesema hakuhusika na ukatili uliofanywa na kundi lake la waasi huko mashariki mwa Congo 2009.

Kwa mujibu wa VOA alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC huko The Hague leo.

Aliwambia majaji kuwa amepigania haki na unyonyaji wa binadamu maisha yake yote na kuiomba mahakama kumwachia huru.

Kiongozi huyo mwenye mwenye umri wa miaka 47 ameshitakiwa kwa makosa 11 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliotokana na vitendo vya kundi lililoko Congo la Democratic Forces for the Liberration of Rwanda. (FDLR).

"