Jan 30, 2011

Mubarak bado atamba lakini aahidi kubadili mawaziri

Mubarak bado atamba lakini aahidi kubadili mawaziri: "

Wamisri waishio Washington Dc wakiandamana kuelekea White house wakitaka msaada wa Obama. Katika hatua isiyo ya kawaida lakini ya kutegemewa kiongozi wa Misri Hosni Mubaraka amezungumza na taifa hilo katai kati ya ghasia zinazoendelea akisema yeye bado ni kiongozi .

Akionyesha ukaidi na kujiamini kiongozi huyo ameweka marufuku ya kutembea usiku na kuwaonya raia wake kuwa ghasia hazitawasaidia kitu.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika maelfu ya wamisri walijazana katika mitaa ya nchi hiyo Ijumaa baada ya sala ya Ijumaa wakizidisha shinikizo kwenye maandamano wakidai kumalizika kwa utawala wa Hosni Mubarak wa miaka 30.

Ghasia ziliripotiwa huko Suez na Alexandria na maeneo mengine kadhaa ya Cairo. Shirika la habari la reuters limeripoti kuwa mwili wa mmoja wa waandamanaji hao ulibebwa katika mitaa ya Suez na waandamanaji wenye hasira.

Shirika la AP limeripoti kwamba mshindi wa tuzo ya Nobel na mwanaharakati wa Misri Mohamed El Baradei yuko kwenye kifungo cha nyumbani. Awali shirika hilo la habari lilisema maafisa wa Misri walimshambulia kwa mabomba ya maji El Baradei mkuu wa zamani wa nishati ya atomiki ambaye alirudi Misri kutoka Austria alhamisi akisema angependelea kuongoza vugu vugu la upinzani.

Imeripotiwa mtoto wake Gamal ambaye amekuwa akizungumziwa kuandaliwa kuwa rais ajaye yupo London na mkewe yupo nje ya nchi kwa hiyo kama akiondoka haijulikani nani atachukua nchi.

Nao wamisri waioshio hapa Washington Dc nao wameandamana kuelekea White house kumtaka rais Obama achukue hatua na kumtaka rais Hosni Mubaraka aondoke madarakani.

"