Mar 2, 2011

CCBRT YAKABIDHI VIFAA VYA WALEMAVU KWAAJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI NA KUIMARISHA ELIMU MAALUMU

 Timu ya Halmashauri ya wilaya ya Mbozi iliyofika kupokea vifaa ikiwa ni msaada kutoka CCBRT kwaajili ya shule maalumu Mbili kati ya tatu zilizopo katika wilaya ya Mbozi ambazo zimekuwa zikipokea na kuwaendeleza watoto wenye mahitaji maalumu!. Wa kwanza ni Bi Simkoko Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwenge, Achor wa Blog Danny Tweve -Mratibu wa shughuli za kudhibiti UKIMWI wilaya, na Afisa Elimu wilaya Bwana Gift Kyando
 Meneja mradi wa kuwezesha walemavu na mapambano dhidi ya UKIMWI kupitia CCBRT CREMENT NDAHAMI akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika mjini Mbeya
Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa  Bwana Mwandepa kutoka sektretalieti ya Mkoa (Afya) akitoa hotuba ya kukabidhi vifaa hivyo kwa wilaya tano za mikoa ya Mbeya na Njoluma kati ya wilaya 15 zinazotekeleza mradi huo kupitia ufadhiri wa PEPFAR ambapo CCBRT kupitia tafiti zilizofanywa kwa ushirikiano na TACAIDS walibaini haja ya kuwepo mradi unaolenga kuzuia maambukizi kwa kundi la walemavu tangu ngazi za mashuleni.
 Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Rungwe bwana Mahenga akipokea vifaa vilivyotolewa kwaajili ya shule za Katumba songwe na Lupata ambazo hutoa mafunzo kwa watoto wenye mahitaji maalumu (wasioona, na walemavu wa viungo). Mashine  ya Transforming yenye thamani ya Tshs 15 Milion ilikabidhiwa kwa wilaya ya Rungwe na Mbili kwa wilaya ya Njombe.

 Timu ya Halmashauri ya wilaya ya Mbozi ikiongozwa na afisa elimu ya msingi  Bw. Gift Kyando wakipokea vifaa vilivyotolewa kwaajili ya shule mbili za Tunduma na Mwenge.
 Nashukuru sana! msaada huu utatusaidia katika kuimarisha utoaji elimu kwa kundi lengwa hasa kwa kuzingatia changamoto za kukosekana kwa  vifaa kwa walemavu  na kusababisha wakati mwingine tushindwe kutunga mitihani ya majaribio kwa kundi hili.
 Ikafuatia fulsa ya wilaya ya Njombe
Ikaja zamu ya Mamlaka ya mji mdogo wa Njombe