Mar 19, 2011

Waziri Nchimbi Awapongeza CHANETA , CHANEZA Kwa Kumaliza Tofauti

Kushoto ni mwenyekiti wa Chaneta Anna Bayi katikati ni Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Emanuel Nchimbi akiwa na Naibu waziri Fenela Mkangara wakati walipotembelea ofisi za CHANETA
Waziri wa Habari Vijana utamaduni na michezo Emanuel Nchimbi amewapongeza CHANETA na CHANEZA kwa kumaliza migogoro yao ambayo ilikuwa haisaidii kuinua kiwango cha mchezo wa netiboli hapa nchini. Nchimbi amewataka CHANETA kuondoa tofauti zao ili kulinda muungano wa Tanzania Bara na Visiwani kwa faida ya wananchi,amesema migogoro haina faida katika michezo zaidi hupunguza hadhi ya mchezo wenyewe. Amesema Serikali ipo kuhakikisha michezo nchini inapiga hatua hivyo kwa kushirikiana na vyama vya michezo serikali ipo tayari kusaidia kila mchezo ili kurudisha hadhi kama ilivokuwa zamani amabapo Tanzania ilikuwa ikisifika kwa umahiri wa michezo aina mbali mbali.
"