May 28, 2011

KOCHA WA MAPINDUZI JUMA MWAMBUSI AVUNJA REKODI KWA KUCHUA UBINGWA MARA MBILI MIKONONI MWA MWANZA



Kijana Juma Mpola akionyesha makeke yake, alikuwa mchezaji wa majimaji katika msimu unaomalizika na ni kijana wa Simike jijini Mbeya ambaye katika mashindano Kili Taifa Cup amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa jumla wa mashindano hayo
 Na Danny Tweve Mbeya.

Kocha wa Mapinduzi starz Juma Mwambusi, leo amevunja rekodi baada ya kuiwezesha timu yake kuifunga Timu ya Mkoa wa Mwanza( Mwanza Herous) kwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali wa Kili Taifa Cup uliochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Hii ni mara ya pili kwa Mwambusi kuwafunga  Mwanza katika fainali za mashindano haya baada ya kufanya hivyo kwa mara kwanza mwaka 2005.

Timu hizo zilipokutana katika fainali iliyochezwa katika uwanja wa jamhuri mjini Morogoro, Mbeya iliweza kuwafunga Mwanza kwa mikwaju ya penarti 4-3.

Mwaka jana Mbeya iliondolewa mapema katika mashindano hayo pasipo kumtumia kocha huyo dalili za wazi zinazoonyesha kuwa mzizi wa Mapinduzi Starz anao yeye.

Mbeya kwa mara ya mwisho iliingia fainali za mashindano hayo mwaka 1966 wakati huo mashindano haya yakiitwa Taifa CUP  baada ya kufungwa bao 1-0 na Timu ya Kilimanjaro katika mchezo mkali uliochezwa katika uwanja wa Kumbumbuku ya Karume zamani ukiitwa Ilala stadium.

Ushindi wa Mbeya ulionyesha dhahiri katika mchezo wa leo ambapo kulikuwa na mashambuzi ya mara kwa mara kwenye lango la timu ya Mwanza, hata hivyo uimara wa ngome ya Mwanza uweliza kupunguza madhara kwa kiwango kikubwa kwa kuwazuia mapinduzi wasipate bao la ushindi mapema.
Hadi  timu hizo zinakwenda mapumziko, hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzake.

Hazta hivyo hali ya mchezo ilibadilika baada ya timu ya mapinduzi starz ya Mbeya kukianza kipindi cha pili kwa nguvu na hivyo kuwabana wapinzani wao katika nusu yao ya uwanja kwa kipindi kirefu.

Alikuwa ni mshambuliaji asiyekata tamaa na mwenye uchu wa magoli Gaudensi Mwaikimba ambaye ametwaa tuzo ya mfungaji bora, kuwainua mashabiki wachache wa mbeya kwenye viti katika dakika ya 88 baada ya kuunganisha kwa kichwa  wavuni  mpira wa krosi iliyopigwa na Juma Mpola  kutoka wingi ya Kulia na kumuuacha kipa wa Mwanza akichupa pasipo mafanikio.

Ikumbukwe kuwa Juma Mpola ametwaa shilingi Milion 2.5  baada ya kuchaguliwa kama mchezaji bora wa jumla katika mashindano hayo huku Mwaikimba naye akitwaa nafasi ya mfungaji bora wa mashindano hayo  kwa kufunga mabao 8 na kumwacha mpinzani wake Jerson Tegete wa Mwanza Herous aliyeambulia kufunga magoli sita tu.

Kutokana na hilo Mwaikimba amejizolea kitita cha shilingi Milion 2.5 na kuisadia pia timu yake ya mapinduzi kutwaa zawadi ya shilingi  Milion 40 kama mabingwa wapya wa Kili Taifa cup kwa mwaka 2011.

Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya soka mkoani Mbeya Ggeorge Chanda mashindano ya mwaka huu yalikuwa na ushindani wa hali ya juu ambapo kila timu ilikuwa inajitahidi kadiri ya uwezo wake kuweza kuchukua kombe hilo, hata hivyo bahati imewaangukia Mbeya ambao wameonyesha ni timu bora kwa kutwa taji hilo.
Kocha Juma Mwambusi ambaye ameonekana kuwa na nyota nzuri na timu ya Mapinduzi Starz pia aliiwezesha klabu ya  Tukuyu staz kucheza katika nane bora katika ligi kuu ya mwaka 2001 na pia kutwaa zawadi ya timu yenye nidhamu bora.