May 7, 2011

MRADI WA UWEZO -TENMET WATUA ILEJE

Hii ndiyo njia panda unapokaribia Ileje ambapo barabara ya kulia inaelekea ofisi za Mkuu wa wilaya na ile iliyoongoza moja kwa  moja inaelekea kwenye mji wa Ileje-Itumba


Haya ni mingoni  mwa mabango kabla hujaingia Ileje


 Darasa nililokuwa nikilijengea uwezo juu ya kuendesha utafiti wa tathmini ya uwezo wa watoto walio na umri wa kuwa shule katika kusoma, kuhesabu na kingereza katika wilaya ya Ileje utafiti unaofanywa kupitia Mradi wa Uwezo chini ya Mtandao wa elimu Tanzania TENMET- kwa wilaya ya Mbeya, Kyela na Mbarali shirika la ELIMISHA ndilo linaloendesha utafiti huo kwa niaba ya mradi wa UWEZO.
Somo likikolea utagundua tu usikivu wake

Role Play ni eneo muhimu la kupima uwezo wa washiriki katika kutekeleza yale waliyofundishwa, hapa wakijaribu kuonyesha namna watakavyofanya utafiti katika jamii

Mapozi ya Picha nayo yamo, hapa washiriki wakifuatilia majadiliano na mada zilikitolewa katika mafunzo yao ya siku mbili yaliyoendeshwa kuanzia ztarehe 3 hadi 5 wilayani Ileje na baadaye kuingia kutekeleza utafiti huo katika vijiji 30,. Jumla ya washiriki 60 walipata mafunzo hayo.