May 8, 2011

HOSPITALI YA MKOA SASA YAJIIMARISHA KUTOA HUDUMA BORA

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambaye ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo Dr HARUNI MAGORI akizungumza nami katika mahojiano maalumu wakati nikiandaa makala ya huduma za jamii na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya nne katika mkoa wa Mbeya jana.

Hii ndiyo moja ya majengo mapya yaliyojengwa kwa msaada wa serikali ya Marekani katika hospitali ya mkoa wa Mbeya ambalo hutumika kama Maabara ambalo nililitembelea jana na kulipiga picha kama inavyoonekana- Picha kwa hisani ya wwww.dtwevetz.blogspot.com

Bibi kikongwe huyu alikutwa na kamera yetu akiwa wodini katika moja ya wadi za wanawake katika hospitali ya Mkoa wa Mbeya, kwa ujumla usafi wa Mablanketi, Vitanda, Shuka na hata vyoo vyake vinaashiria kuongeza matumaini kwa wagonjwa achilia mbali huduma ambazo zinazidi kuboreshwa siku hadi siku.

 Bibi alipoona kamera kama imemshtukiza hivi, akatafuta pozi la pili na akaomba picha nyingine ya kumbukumbu!!!nikamfotoa, tabasamu kidogo bibi eeeeee!!! http://www.dtwevetz.blogspot.com/
Timu ya watendaji katika wadi ya akina mama ikiwa imepozi kwa picha wakati nikidocument  mazingira ya hospitali ya Mkoa wa  Mbeya iliyopo eneo la Forest mjini hapa. Kwa ujumla hospitali hiyo kwa sehemu kubwa imechangiwa na fedha zinazotengwa na mkoa kupitia ofisi ya katibu tawala katika kuwezesha huduma za tiba kwa wananchi wake. Kwa sasa inakadiriwa kuwa na vitanda zaidi ya 100 na inaendelea kupanuliwa majengo yake kwa kujenga majengo mapya ili kutoshereza mahitaji. Wastani wa wagonjwa wa nje kwa siku ni zaidi ya 80 ambao hufika kupata huduma hapo.picha zote na indaba africa.