May 8, 2011

SASA APOLO YA INDIA YAANZISHWA NYINGINE MBEYA

Mashine maamlumu inayopima mirija ya kusukuma damu kwa wagonjwa wanaofika kupima tatizo  la moyo. Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Moyo Dr Haruni Magori, mashine hiyo ni miongoni mwa mashine za kisasa nchini ambayo imetengenezwa mwaka 2009 na baada ya uchunguzi wa mgonjwa kufanyika taarifa zake hupokelewa moja kwa moja katika kituo kimoja cha marekani ambapo uchunguzi zaidi wa tatizo hutafsiriwa na hatimaye majibu kupatikana baada ya saa kadhaa kupitia computer zinazoambatana na mashine hiyo.
 Hapa nikijiandaa kwa mahojiano na Dr Magori kwa kumwekea wire less microphone katika hatua za awali za kutengeneza documentary ya masuala ya tiba ya magonjwa sugu nchini na Ugonjwa wa Moyo ukiangaziwa ambapo kwa mujibu wa Dr MAGORI asilimia 40 ya wagonjwa wanaofika kupata huduma za tiba katika vituo mbalimbali mkoani humo wana tatizo la moyo pia.
 Hapa akionyesha namna mashine hiyo inavyofanya kazi kwa kuonyesha mapigo ya moyo wa binadamu na namna msukumo wa damu unavyofanyika kupitia pampu  zilizomo mwilini

 Hiki ni kiti maalumu ambacho pia hudumika kupima mishipa iliyokufa (hasa wale wanaopooza baadhi ya viungo) imeunganishwa na mfumo wa umeme ambapo mkononi mwake ameshikiria remote ambayo ndiyo hutoa matokeo ya eneo lipi hasa limepoteza mawasiliano mwilini!
Hii ndiyo Klinini ya Afya Speciliazed Clinic iliyopo mtaa wa soko la Makunguru na Kabwe ambayo imeendelea kutoa huduma kwa wananchi wa mikoa ya nyanda za juu kusini  ambapo takwimu zinaonyesha kuwepo kwa ongezeko kubwa la wagonjwa wa matatizo ya moyo , ambao kulingana na Dr magori yanaina mbalimbali zaidi ya sita.
 Kinachoonekana kwenye kopyuta hapo ni uvimbe uliomo kwenye moyo wa mmoja wa wagonjwa waliochunguzwa na kituo hicho ambapo taarifa zake zilipelekwa marekani na baadaye zikarejeshwa kwenye mfumo wa mashine hiyo zikiwa zimetafsiriwa zikionyesha urefu wa sentimeta kadhaa za uvimbe huo unaoonekana kwenye ncha za vidole hapo!!