Jun 12, 2011

KUFUTWA kwa onyesho la Mwanamuziki Hugh Masekela

BENKI ya Stanbinc inasikitika kufutwa kwa onyesho la mwanamuziki kutoka Afrika Kusini lililotegemewa kufanyika usiku wa jana Jumamosi kwenye hoteli ya Golden Tulip Dar es Salaam.
Onyesho hilo lilifutwa kufuatia mwandaaji ambaye ni Heri Bomani na Kamapuni yake ya Full Circle Africa Limited kushindwa kumlipa msanii kama walivyokuwa wamekubaliana awali.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika muda mfupi leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Abdallah Singano alisema “Tunasikitika sana kwa kufutwa onyesho hili ambalo tulikuwa tumedhamini tunategemea kuchukua hatua za kisheria kwa mwandaaji na Kampuni yake”.
Naye Mwanamuziki mwenye heshima kubwa ndani na nje ya Bara la Afrika Hugh Masekela alieleza kuwa amesikitishwa kutokana na mambo yalivyotokea.
“Tunasikitika sana kuja Dar es Salaam na kushindwa kufanya onyesho kama tulivyokuwa tumepanga kutokana na mwandaaji kushindwa kutimiza makubaliano yetu,
Tunaomba radhi kwa mashabiki wetu ambao walikuwa wamejitayarisha kuja kwenye onyesho hilo lakini napenda kuwaambia kuwa tutarudi tena Tanzania kufanya onyesho hapo baadaye” alisema Masekela.
Naye Singano aliendelea kwa kusema kwamba “Tunaomba radhi kwa mashabiki wote wa Hugh Masekela walionunua tiketi kuona onyesho hilo na hatimaye kufutwa”.
Singano anamalizia kwa kusema kuwa kwa wale wote walionunua tiketi za onyesho hilo wamtafute mwandaaji ili aweze kuwarudishia fedha zao. CHANZO. MICHUZI BLOG
"