Jun 13, 2011

MKUTANO WA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII MKOA MBEYA


Maafisa maendeleo ya jamii wa wilaya za mkoa wa Mbeya pamoja na waratibu wa shughuli za kudhibiti UKIMWI katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya wakiwa pamoja na mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Betha Swai, na maofisa wa sekretalieti ya Mkoa wa Mbeya kwenye eneo la Maendeleo ya Jamii, Mratibu wa TACAIDS mkoa na Mipango baada ya kufungua Mkutano huo wa siku Mbili unaolenga kurejea majukumu ya Maendeleo ya jamii na Mapambano dhidi ya UKIMWI katika wilaya hizo


Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya  Betha Swai akizungumza na maafisa maendeleo yajamii mkoani Mbeya leo.

Maafisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya za Mbozi na Ileje wakinukuu sehemu ya maelekezo ya katibu Tawala Mkoa wa Mbeya

Washiriki wa mkutano huo wakiwa busy kunote vitu kwenye mkutano huo

Naam kati ya mengi aliyoyazungumza Bi Swai Katibu tawala mkoa wa Mbeya, amesema miongoni mwa dhambi zinazowakabili maafisa hao ni kushindwa kusaidia wananchi katika kuleta mabadiliko na badala yake kuisaliti NCHI ya Tanzania na matokeo yake kuwa washangiliaji na wahubiri wa Nchi ina raslimali nyingi lakini wananchi bado maskini, kumbe jukumu kubwa ilikuwa ni kuwadilisha wananchi ili raslimali hizo wazione namna zinavyoweza kutumika kuondokana zna umaskini.