Jun 21, 2011

LAUNCHING OF SAPPHIRE PROGRAM IN MBEYA REGION TODAY

Stake holders from  various community groups and Government entity listerning to panelists presenting  the program  focus and strategies  to be followed during the implementation of Storage and Proper Post Harvest Improvements of Resource Efficiency -SAPPHIRE which is financed  and implemented in collaboration between AGRA(financing)  and TECHNOSERVE(Implementer) . The program will work on Maize and  Paddy crops in Mbeya -selected three districts being Mbozi, Kyela and Mbeya Rural

 Wadau wakieendelea kuchakata mpango wa namna bora ya kuhifadhi mazao baada ya mavuno na namna ya kutumia mfumo wa stakabadhi maghalani unaotekelezwa kwa mazao mawili ya Mpunga na mahindi katika wilaya za Mbeya, Mbozi  na Kyela kuanzia mwezi January 2011 hadi January 2013. Mradi uznaztarajia kutumia zaidi ya dola za kimarekani 1.5 Milion kwa kipindi hicho cha miaka miztatu ambapo utawezesha ujenzi wa maghala 20 na kuwawezesha wakulima wadogo 20,000 katika mkoa wa Mbeya kuongeza thamani ya mazao yao kupitia program ya access to market kupitia mnyororo wa thamani
Mkurugenzi Mkazi wa TECHNOSERVE TANZANIA Bi Hillary Miller-Wise akielezea mpango wa SAPPHIRE katika mkoa wa Mbeya zna mtazamo wake katika harakati za kuwaondoa wananchi kwenye umaskini.

Julius Kallambo Mtaalamu wa Mpango wa stakabadhi ya mazao Gharani -AMSDP Arusha akizungumzia nafasi za Mabenki kuwa wabia muhimu wasio na masharti ya kuangalia faida peke yake  katika uendeshaji wa mfumo huo, na badala yake kuwa na mtazamo pia wa kushiriki hata kwenye hasara inapotokea mkulima ameathirika na soko.

Joseph Marco -Afisa Kilimo wilaya ya Kyela akitoa uzoefu wake ambapo amesema mpango huo unahitaji kwanza kujenga msingi imara katika makundi ya watendaji wakiwemo wagani kwenye ngazi za jamii, wakulima wenyewe na viongozi wengine ili waweze kuuhubiri mpango wa stakabadhi mazao gharani kwa hali ambayo haitatofautiana kutoka eneo moja na jingine