Jun 17, 2011

UCHAGUZI CHADEMA MKOA WA MBEYA WAPIGWA KALENDA, KISA MALALAMIKO

Uchaguzi wa Chadema Mbeya umeahirishwa sababu kubwa ni pingamizi.


Uchaguzi uliokuwa unatarajia kufanyika Juni 20 mwaka huu kunmchagua Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) umeahirishwa.

Kuahirishwa kwa uchaguzi huo kumethibitishwa na Katibu wa Chadema mkoa wa Mbeya Eddo Mwamalala ambaye amesema kuwa amepata maagizo ya kusimamisha uchaguzi huo mpaka hapo baada ya mwezi mmoja.

''Makao makuu wamepokea malalamiko yaliyopelekwa na wagombea hivyo mpaka wajiridhishe na kwamba watatoa taarifa baada ya mwezi mmoja baada ya kujiridhisha'' amesema Mwamalala.