Jun 17, 2011

MAMA ANNA ABDALAH AMSAFISHIA NJIA 2015 UBUNGE JOHN MNYIKA


Asubuhi ya leo katika kipindi cha JAMBO TBC walikuwepo mh. anna abdalah na Mh. Mnyika wakijadili taratibu za kunge kuhusu miongozo ya spika. Mh. anna abdalah alimsifia sana mnyika kuwa ni mbunge makini, msikivu na anayetoa hoja za nguvu na sio nguvu ya hoja. akasema anamwombea aendelee kuwepo ndani ya bunge kwa muda mrefu kwani atakua mfano mzuri wa kuigwa na vijana wengine.

Akizungumzia hali ya kushambuliana bungeni alisema, kimsingi inahitaji kukemewa kwakuwa wabunge wote wanawakilisha maslahi ya watanzania wote wakati ambapo miongoni mwao wanajitutumua kuwasilisha maslahi ya vyama vyao kinyume kabisa na uwepo wao katika mazingira ya Bunge.

alisema inapokuwa bungeni wabunge wote wanatakiwa kusahau maslahi ya vyama vyao na kuweka utaifa mbele na maslahi ya taifa kwa ujumla lakini hivi sasa kumeibuka uvyama bungeni hali ambayo inaharibu kabisa mtazamo mpana wa chombo hicho katika kusimamia maslahi ya taifa.