Jun 5, 2011

WAZEE WA THE MUSHROOM WATOA SIRI YA KUENDELEA KUWEMO KWENYE GEMU

Kundi la The mashroom likifanya mahojiano na Mwandishi wa K24 katika moja ya vipindi vilivyorekodiwa hivi karibuni ambapo kundi hilo limetoa siri ya kuendelea kuwemo kwenye Gem wakati makundi mengine yanazimika kwa kasi kutokana na vifo vya waimbaji wake kuwa ni kutokana na misingi waliyojiwekea ya kujali afya zao kwa kutoshirikisha na vitendo vya Ulevi, Ngono na matendo yanayopunguza uhakika wa maisha ya mtu. Kundi hilo limedumu kwa miaka 40 sasa tangu lianzishwe na makazi yake ni Mombasa nchini Kenya. Utakumbuka Nyimbo za Embe dodo, Harambee, nk

Kiongozi wa Kundi hilo ambaye anaimba na mdogo wake, kimsingi kundi hilo awali lilikuwa la wanandugu lakini baadaye wakaunganishwa watu wengine na sasa bado wanaamini kuwa ni ndugu kwakufanya kazi pamoja na kuendelea kuendesha familia zao.