Jul 13, 2011

FINAL ZA MASHINDANO YA NGOMA YA BALIMI EXTRA LAGER 2011

Kiongozi wa kundi la Rugowoile kutoka mkoani Kagera akichekelea kitita cha Tsh. 1,000,000/= baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi wa mashindano ya Ngoma ya Balimi Extra Lager Kanda ya ziwa, Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mwanza Bw. Patrick Karangwa. Nafasi ya pili ilishikwa na Utandawazi toka Mwanza na kujipatia kitita cha Tsh. 750,000/= na cha tatu ni Mwenge Sanaa Group toka Tabora na kujipatia kitita cha Tshs. 500,000/=.
Fainali za Mashindano ya Ngoma ya Balimi Extra Lager, zimefanyika Jumamosi tarehe 9/7/2011 katika uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza na kufanikiwa kupata kundi la Rugowoile kutoka mkoani Kagera kutawazwa rasmi washindi wa mashindano hayo na kujinyakulia kitita cha Tsh. 1,000,000/=
Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha jumla ya vikundi kumi kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Shinyanga, Mara na Tabora, mshindi wa pili ni kundi la Utandawazi kutoka mkoani Mwanza ambao wameondoka na donge nono la Ths. 750,000/= Mshindi wa Tatu ni kundi la Mwenge Sanaa Group kutoka mkoani Tabora ambao wameondoka na kitita cha Tahs. 500,000/=, Mshindi wa Nne ni kundi la Rugu kutoka mkoani Kagera ambao wamejinyakulia donge nono la Tsh. 400,000/= Mshindi wa Tano hadi wa Kumi wamejinyakulia kitita cha Tsh. 300,000/= kila kundi.
Kundi la Egumba Sanaa Group toka Mara likionyesha umahiri wake.
Burudani zikiendelea.
Kundi la Utandawazi toka Ukerewe wakionyesha umaarufu wao kumiliki jukwaa ambapo kundi hili lilishika nafasi ya pili katika fainali hizo.
Kundi la Mwenge Sanaa Group toka Tabora likitimbwilika na ngoma za asili kupitia bia ya Balimi Extra Lager. Walishika nafasi ya tatu na kujinyakulia Tshs 500,000/=.
Kundi la Mang’ombega kijiji kutoka Mwanza, likiingia tayari kuonyesha manjonjo yao ndani ya uwanja wa ccm Kirumba katika mashindano ya ngoma ya Balimi Extra Lager.
Kundi la Kiwajaki kutoka Mkoani Mara, likitoa ujumbe wa Bia ya Balimi Extra Lager. KUTOKA MTAA KWA MTAA