Jul 13, 2011

MADEREVA WA MAROLI NCHINI WATANGAZA MGOMO USIO NA KIKOMO KUANZIA JULY 17 MWAKA HUU

Mwenyekiti wa muda wa Madereva wa maroli yanayofanya safari zake nje ya nchi  MOHAMED FIKIRI akisoma msimamo wa chama hicho baada  ya kupeleka malalamiko yao kwa waziri Mkuu bila kupatiwa majibu, hapa alikuwa akizungumza jana na mtandao wa indaba africa katika kituo kikuu cha maroli cha Sogea -Tunduma ambako walikutana jana kujadili maendeleo ya mipango yao ya Mgomo nchi nzima.

Mmoja wa madereva waliozungumza na Indaba africa bwana Abdallah Juma Idd  ambapo ametaja miongoni mwa malalamiko yao kuwa ni pamoja na kulipwa pesa za madafu wakati nchi zote wanakopita matumizi yake yanaenda kwa dola.

Bi Mkubwa Mama lishe wa eneo la Gogea Bi Chema Yahaya akizungumzia ugumu wa biashara zao kutokana na kukopwa na madereva wa magari makubwa yanayovuka eneo la Mpakani Tunduma ambapo amesema wakati mwingine imefikia wameshindwa kuendelea kutoa huduma za mama Lishe

Dereva Mohamed Salumu akizungumza na indabaafrica juu ya malalamiko yao kwa kutopatiwa mikataba ambapo alituhumu kuwa hali hiyo inatokana na baadhi ya vingunge wa serikali kuwa na hisa katika makampuni ya usafirishaji ambapo wamekuwa wakikwepa kufanya maamuzi  magumu ya kuwa na mikataba na madereva wao.

Madereva zaidi ya 500 waliokusanyika hapo wakishangilia jambo katika kikao hicho

Moja ya kero wanayolalamikia ni vumbi katika eneo la Sogea ambapo mmoja wao aliamua kutoa mfano kwa kupitisha roli lake kwaa staili hii! Picha zote na Indaba africa