Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa tuzo na Waziri Mkuu wa Antigua and Barbuda Mh. Winston Baldwin Spencer kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya afya, teknolojia na maendeleo kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na taasisi ya South-South katika hoteli ya Waldorf Astoria jijini New York Jumatatu usiku.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiikabidhi tuzo hiyo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe baada ya kuipokea. Nyuma ya Mh. Membe ni Balozi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa Mh Ombeni Sefue (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh Mwanaidi Maajar
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa shukrani kwa kupewa tuzo hiyo. Marais Paul Kagame wa Rwanda, Abdoulaye Wade wa senegal na Mwai kibaki wa Kenya, pia walipokea tuzo kwa michango yao katika maendeleo ya nchi zao
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipewa shada ya maua kama pongezi kwa kupokea tuzo
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Dkt Marion Bergam, Mkurugenzi wa miradi ya Health Care Projects ya Miracle Corners of the World katika mkutano wa kwanza wa kuhimiza hatua zichukukuliwe dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza, hususan ya kinywa. Serikali ya Tanzania ndiyo iliyodhamini mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha New York kitivo cha meno
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa hafla ya kupongeza mafanikio ya juhudi za kupambana na ugonjwa wa malaria ya Roll Back Malaria katika hoteli ya Intercontinental jijini New York
Sehemu ya umati uliohudhuria hafla hiyo ya Roll Back Malaria
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Dkt Asha Rose migiro kwenye hafla hiyo ya Roll Malaria
Mwanamuziki maarufu wa Afrika Kusini ambaye ni Balozi wa heshima wa Roll Back Malaria Yvonne Chakachaka akiendesha shughuli hiyo kama MC
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kihutubia mkutano wa kuhamasisha utokomezaji wa magonjwa ya Kinywa katika kitivo cha tiba ya Meno cha Chuo Kikuu cha New York. Mkutano huu uliandaliwa na kudhamini na Serikali ya Tanzania na wafadhili-wenza ambao ni Serikali za Australia, Sweden na Shirika la Afya Duniani (WHO)
Sehemu ya ujumbe wa Watanzania kutoka sekta ya utalii
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa zanzibar Mh Juma Duni Haji (kati) na wasaidizi wake kwenye hafla hiyo
Wahudhuriaji wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kutoa mada yake ya ufunguzi
Meza kuu inasimama kupiga makofi baada ya mkutano huo
Madaktari Bingwa kutoka Wizara ya Afya na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakisubiri kugawa vipeperushi kwa wanaoingia mkutanoni
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa Makame Mnyaa Mbawala (kati), Waziri wa Maliasili na Utalii (shoto) pamoja na Mbunge wa Bukombe, Profesa Kulikoyela Kahidi wakiperuzi maandiko kuhusiana na mkutano huo wa kuhamasisha vita dhidi ya magonjwa ya kinywa
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Mama Blandina Nyoni (kushoto) na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt Deo Mutasiwa wakipozi na Dkt Marion Bergman (kati) wakati wa mkutano huo wa kuhamsasisha kuchukuliwa kwa hatua kutokomeza magonjwa ya kinywa
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na wenzie wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mama Hilary Clinton alipokuwa akifungua mjadala wa maendeleo ya wanawake katika kujiendeleza kwa Kilimo katika hoteli ya Intercontinental jijini New York
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na wenzie katika mjadala uliofunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mama Hilary Clinton kuhusu maendeleo ya mwanamke katika kujiendeleza kwa Kilimo katika hoteli ya Intercontinental jijini New York
Umati wa watu katika Mjadala huo
Jedwali la ALMA lililozinduliwa Jumatatu lenye kutoa dira na namna kila nchi wanachama wanavyopambana na ugonjwa wa Malaria
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihojiwa juu ya maendeleo ya mpango huo wa ALMA
Mmoja wa waliohudhuria hafla hii akipitia jedwali la African Leaders Malaria Alliance (ALMA)
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa Jedwali la uwajibikaji na kuchukua hatua dhidi ya ugonjwa wa malaria uliondaliwa na taasisi ya viongozi wanaopigana kuondoa malaria Afrika ya African Leaders Malaria Alliance (ALMA) ambayo yeye ndiye mwenyekiti wake. Pamoja naye meza kuu ni viongozi wa juu wa ALMA, Benki ya Dunia, WHO na Umoja wa Mataifa
KUTOKA IKULU MAWASILIANO BLOG