Oct 12, 2011

HALMASHAURI YA NAMTUMBO YAWAPIGA TAFU WANAWAKE KUPATA MITAJI YA KIUCHUMI

Mhasibu wa Namtumbo muungano saccos ya wilayani Namtumbo Bi Mwanahamis Malk (kushoto) akipokea hundi ya tsh 5ml kutoka kwa mkuu wa wilaya hiyo,Savery Maketta zilizotolewa na halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya kuviwezesha vikundi mbalimbali vya uzalishaji mali,kushoto ni mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya Bw Mussa Zungiza.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,Savery Maketta akitoa nasaha kwa viongozi wa vikundi vya akina mama wa wilaya hiyo baada ya viongozi hao kukabidhiwa fedha na halmashauri ya namtumbo, kwa ajili ya kuwakopesha wana vikundi wenzao jana,kushoto ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw Mussa Zungiza.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Mussa Zungiza kushoto,akiongea na wawakilishi wa vikundi vya akina mama wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,kabla ya kukabidhi hundi kwa ajili ya kuviwezesha vikundi hivyo jana mjini namtumbo,kulia ni mkuu wa wilaya hiyo Savery Maketta.
viongozi wa vikundi vya akina mama kutoka wilaya ya namtumbo Ruvuma,wakimsikiliza mkuu wa wilaya hiyo Savery Maketta,hayupo pichani kabla ya kukabidhiwa hundi zao kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wao,ambapo kila kikundi kilikabidhiwa kati ya 5ml hadi 7 ml na halmashauri ya wilaya hiyo jana mjini namtumbo.Picha na Muhidin Amri-Songea