Oct 12, 2011

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL ATOA POLE MSIBA WA MTOTO WA BALOZI JUMA MWAPACHU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mke wa Balozi Juma Mwapachu, Rose Mwapachu, wakati alipofika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam jana oktoba 11, 2011, kumpa pole kufuatia kifo cha mtoto wake, Harith Mwapachu, kilichotokea jana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha (CHADEMA) Freeman Mbowe, wakati walipokutana katika msiba wa mtoto wa Balozi Juma Mwapachu, Harith Mwapachu, Mikocheni jijini Dar es Salaam jana Oktoba 11.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waombolezaji, wakati akiondoka nyumbani kwa Balozi Juma Mwapachu, wakati alipofika kutoa pole kufuatia kifo cha mtoto wa Balozi Juma Mwapachu, Harith Mwapachu jana Oktoba 11.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha maombolezo cha Harith Mwapachu, ambaye ni mtoto wa Balozi Juma Mwapachu, aliyefariki dunia jana Oktoba 11, 2011.Kulia ni Balozi Juma Mwapachu.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais