Nov 15, 2011

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL APOKEA MADAI YA WANANCHI KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI, KUELEKEA MKUTANO WA DURBAN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Madai ya Wananchi ya Namna ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi, kutoka kwa Mwanaharakati wa Mabadiliko ya tabia Nchi, Laurence Chuma, wakati wa Kongamano la Msafara wa kuelekea katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi unaotarajia kufanyika Durban Afrika ya Kusini mwezi ujao. Kongamano hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mwakilishi wa Asasi za Mabadiliko ya Tabia Nchi, Rebecca Muna.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa Kongamano la Msafara wa kuelekea katika mkutano wa mabadfiliko ya Tabia Nchi unaotarajia kufanyika Durban Afrika ya Kusini mwezi ujao. Kongamano hilo limefanyika leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Asasi za Mabadiliko ya Tabia Nchi, Rebecca Muna, akizungumza wakati wa Kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakiwa ukumbini humo.
Makamu wa Rais Dkt Bilal (katikati) Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kulia) na Mwakilishi wa Asasi za Mabadiliko ya Tabia Nchi, Rebecca Muna, wakifurahia jambo, wakati wa Kongamano hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo ambao miongoni mwao wanashiriki katika msafara huo kuelekea Durban.