Nov 12, 2011

NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA SIDO YA NYANDA ZA JUU KUSINI MKOANI RUKWA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu (MB) akikata utepe kama ishara ya kufungua rasmi maonyesho ya 9 ya SIDO ya nyanda za juu kusini inayoshirikisha mikoa ya Rukwa, Iringa na Mbeya. Kulia kwake anayeshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana. Maonyesho hayo yanafanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa kwa kushirikisha wajasiriamali kutoka zaidi ya mikoa 14 nchini na wengine kutoka nchi jirani za Kenya na Burundi. Kwa habari zaidi nenda hapa: (http://rukwareview.blogspot.com/)
Mkurugenzi Mkuu wa SIDO nchini Ndugu Mike Laizer akifafanua jambo kwa Naibu wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu kwenye banda la SIDO. Kulia kwa Naibu Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana.
Uhifadhi wa Mazingira nao umepewa kipaumbele Mkoani Rukwa, Mjasiriamali wa uhifadhi wa Mazingira wa kikundi cha REYO akinadi miti aina mbalimbali inayofaa kwa uhifadhi wa mazingira na matumizi mengineyo katika maonesho hayo.
Maonyesho hayo yakiendelea
Mjasiriamali wa Rukwa anayejishughulisha na utengenezaji wa viatu kwa kutumia ngozi mbalimbali. Chipawas Leather Tunning wanapatikana maeneo ya Jangwani Wilayani Sumbawanga, wapo pia kwenye maonesho hayo.
Haya mambo ya ajabu pia yapo, inadaiwa ni Mtu wa ajabu kutoka Burundi aliyezaliwa kichwa kitupu, ana uwezo wa kuzungumza lugha tofauti na wakati wa kumuhoji alidai kuwa chakula chake ni Sindano maalum. Katika akili ya kawaida haifikiriki na wengi wa watu waliomtembelea huyu bwana ikiwa ni pamoja na mimi walisema haya ni MAZINGAUBWE. Huyu bwana anapatikana kwenye banda moja na ili kuweza kumuona inatakiwa kulipia shillingi mia tano tu. Nilishuhudia baadhi ya watoto waliopata bahati ya kumuona wakilia kwa hofu na wengine wakiwa na mshangao mkubwa.
Naibu Waziri akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga. kutoka kwa john Bukuku wa blog ya..