Nov 12, 2011

TABORA YAKUMBWA NA UHABA WA MAFUTA IKIWA LEO NI SIKU YA NNE TATIZO LAWA KUBWA

Uhaba wa mafuta katika mkoa wa Tabora.Hivi ndivyo hali ilivyo katika pita pita za Latest news Tz na kujionea mstari mrefu watu wakisubiri kupata huduma ya mafuta.Hali hii ilianza kama siku nne zilizopita na kila siku kituo kimoja kinatoa huduma hiyo.
Nov12
Written by haki | // 0 comments
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpa tone la dawa ya Chanjo mtoto, Renatha Faustine (1) wakati wa alipokuwa akizindua Kampeni ya Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Polio kwa watoto kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano, Kitaifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Novemba 12, 2011. Aliyembeba mtoto ni mama wa mtoto huyo, Selina Hando Mkazi wa Moshono Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Polio kwa watoto kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano, Kitaifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Novemba 12, 2011.
Watoto wa Shule za Msingi, wakipita mblele ya jukwaa la mgeni rasmi Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mabango yenye ujumbe wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Polio kwa watoto kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano, Kitaifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Novemba 12, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais.