Oct 7, 2012

CHUO CHA MIPANGO SASA KUJIELEKEZA KWENYE MIGOGORO SERIKALI ZA MITAA


Na Danny Tweve
Dodoma 
MAHUSIANO MABAYA BAINA YA MADIWANI NA WATENDAJI KATIKA HALMASHAURI NYINGI ZA WILAYA NCHINI NI SEHEMU YA MATOKEO YA MFUMO WA UGATUAJI MADARAKA AMBAPO UMEFANYIKA PASIPO KUBAINI MAPENGO YA UELEWA KATIKA MAKUNDI HAYO MAWILI IMEBAINISHWA.

HAYO NI SEHEMU YA MATOKEO YA  UTAFITI  WA MAHITAJI YA MAFUNZO ULIOFANYWA NA CHUO CHA MIPANGO DODOMA KWA  HALMASHAURI ZA WILAYA NCHINI, NA KWAMBA KUTOKANA NA CHANGAMOTO HIYO, CHUO KIMEANDAA MTAALA UNAOLENGA KUJENGA UWEZO KWA VIONGOZI WA VIJIJI, KATA NA HATIMAYE  WILAYANI  ILI KUWEZESHA UTENDAJI USIO NA MIGOGORO

WAKIZUNGUMZA KWA NYAKATI TOFAUTI MAKAMU MKUU WA CHUO HICHO SEHEMU YA RASLIMALI WATU NA UTAWALA BW. TIBELIO MDENDEMI NA MKUU WA CHUO HICHO BWANA CONSTANTINO LIFURILO , WAMESEMA SAMBAMBA NA MAFUNZO HAYO, PIA CHUO KINAENDELEA NA UANDAAJI WA TAARIFA ZA USURI WA HALI ZA KIJAMII NA KIUCHUMI ZA WILAYA ZA MKOA WA MOROGORO BAADA YA KUKAMILISHA WILAYA ZOTE ZA MKOA WA DODOMA

CHINI YA MPANGO HUO, HALMASHAURI ZA WILAYA NCHINI KAMA ENEO MUHIMU LA UGATUAJI WA MADARAKA KATIKA  SERIKALI ZA MITAA LIMEWEKEWA MKAZO KATIKA MAFUNZO  HAYO YATAKAYOHUSISHA VIONGOZI WA  KUCHAGULIWA NA WATENDAJI WAAJIRIWA WA HALMASHAUR AMBAPO  WILAYA YA MBULU KATIKA MKOA WA MANYARA   IMETENGWA KAMA ENEO LA MAJARIBIO  NA MPANGO HUO UTATEKELEZWA KWA USHIRIKIANO  BAINA YA CHUO CHA MIPANGO DODOMA NA NA  SERIKALI YA UHOLANZI

DANNY TWEVE DODOMA