Feb 7, 2013

KIMONDO SPORTS CLUB YA MBOZI YAINGIA SITA BORA ZA MKOA MBEYA LIGI DARAJA LA TATU





Matokeo ya soka  kati ya Kimondo fc ya Mlangali wilayani Mbozi na Uwanja wa Ndege ya Mbeya leo yameacha afya za wakazi wa mbozi zikiwa raha mstareheee
Katika mchezo huo Kimondo Fc imeidungua bao 1-0  timu ya wajanja wa mji iliyolea wacheza wengi wanaocheza ligi kuu kwenye timu za Prison, Azam, na zingine nyingi zinazozoshiriki ligi kuu
Wakicheza chini ya hamasa ya diwani wao Erick  Ambakisye, Kimondo ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa imezidiwa mashambulizi na  air port ya Mbeya lakini kipindi cha pili vijana hao walibadilika na kuanza mashambulizi kwa kutumia wingi ya kushoto ambayo yalileta maafa
Ikiwa ni dakika ya 70 vijana wa Kimondo waliweza kuihadaa ngome ya Air port na kujipatia bao pekee lililodumu muda wote wa dakika 90 hivyo kuwawezesha kufikia hatua nzuri ya kuingia timu sita bora katika ligi ya mkoa ambapo sasa zimejihakikishia mazingira mazuri  kufuzu kupanda daraja la pili.
PIGA NIKUPIGE ILIYOTOKEA KWENYE LANGO LA AIR PORT NA HATIMAYE KUZAA GOLI

MASHAMSHAM YA UWANJANI, HAWA NI MASHABIKI WA KIMONDO WAKIZOMEANA NA WALE WA AIR PORT

 MOJA YA JARIBIO BAYA LA AIR PORT LAKINI WAKAKOSA GOLI
 DIWANI WA MLANGALI ERICK AMBAKISYE (MWENYE KAPELO YA CCM) AKISOGEA KWENDA KUTOA USHAURI KWA TIMU YALE AMBAYO ILIIBUKA KWA USHINDI WA BAO 1-0 DHIDI YA AIRPORT YA MBEYA
MNAZI WA TIMU YA KIMONDO AKIZUNGUKA UWANJANI NA BENDERA KUIPA HAMASA TIMU YAKE