Feb 13, 2013

MAHAKAMA KUU INAYOENDELEA NA KIKAO CHAKE MBOZI YAMHUKUMU KUNYONGWA HADI KUFA MSHTAKIWA




MBOZI                                    12, FEB 2013           HUKUMU
Mahakama kuu kanda ya Mbeya imemhukumu  PETER MWAFRIKA mkazi wa  Ndolezi wilayani Mbozi kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia.

Akisoma hukumu hiyo iliyochukua saa 1.30 Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya mbeya  NOEL CHOCHA amesema licha ya mikono ya mahakama kufungwa kutoa adhabu ndogo kwa kosa la maauaji ya kukusudia, pia adhabu hiyo ni hatua ya kukomesha watu wenye tabia kama za mtuhumiwa kujichukulia hatua mikononi mwao.
Akirejea mazingira ya kesi hiyo jaji Chocha amesema mnamo Februaly 11,2010 mshatakiwa na wenzake watatu walifanya kosa la mauaji ya kukudia chini ya kifungu 196 chasheria ya mwenendo wa makosa ya jinai  kwa kumuua KOSAM MWAFRIKA ambaye ni kaka wa marehemu  katika kijiji cha Shaji kwa kumkata koromeo na kulitenganisha vipande viwili.
Jaji Chocha katika maelezo yake alisema mshtakiwa akiwa na wenzake ambao walitoweka baada ya mauaji hayo walimvamia Kosam akiwa na mkewe shambani kwake eneo la Zanzule, Ndolezi na kisha kumkamata marehemu kwa maelezo kuwa walikuwa wametumwa kumkamata ili wampeleke polisi kwa kosa la wizi wa Ng'ombe.

Hata hivyo katika mabishano shambani hapo, marehemu na wenzake walitamka wazi kuwa walikuwa wametumwa kumuua marehemu hivyo kuongeza nguvu za ushahidi wa kumtia hatiani.

sababu za mauaji hayo ni ugomvi wa muda mrefu uliokuwepo kati ya marehemu na mama yake mzazi wa mshtakiwa ambao walikuwa wakigombea ardhi,(wote ni ndugu) na kwamba siku moja kabla ya tukio hilo kulikuwa na kesi katika mahakama ya mwanzo Mlowo iliyokuwa imefunguliwa na Mama mzazi wa mshatakiwa.

Inaelezwa pia kuwa wakiwa njiani kumpeleka polisi, baada ya kubaini kuwa kuna watu wanawafuatilia ghafla mtuhumiwa mwingine (ambaye hakuwepo mahakamani) alimkata marehemu panga la shingo na kumfanya marehemu akose nguvu na kuanguka, hata hivyo kwa kuonyesha kutoridhika na hali hiyo mtuhumiwa aliongezea kwa kumkata marehemu na panga kwenye koromeo na kulitenganisha kabisa.

Jaji kabla ya kutoa hukumu alirejea mazingira ya tukio hilo na kujiridhisha na miongozo, viini vya shauri la mauaji na hoja zilizotolewa na washauri wa mahakama ambapo ilithitika kuwa kulikuwa na dhamira ya mauaji na  tendo la mauaji lilifanyika 

Katika ushahidi wa shauri hilo jumla ya mashahidi watatu waliletwa mahakamani akiwemo kaka wa mshtakiwa ambao wawili kati yao walithibitisha pasipo shaka kwamba mshtakiwa  Peter kuhusika na tukio la kumuua kwakukusudia Kosam .

Katika utetezi wake wakili wa mshtakiwa ZAKIA SULEIMAN aliiomba mahakama impe adhabu nafuu mshtakiwa kutokana na umri wake mdogo hivyo mchango wake kuhitajika katika ujenzi wa taifa, pamoja na kuwa na wategemezi wakiwemo wake wawili na watoto wane.
Serikali iliwakilishwa na Wakili  Rogers Francis

katika hatua nyingine jaji Chocha aliamua kufanya kazi ya kutoa elimu mahakamani humo, akirejea matukio yaliyojitokeza hivi karibuni wilayani Momba na Mbozi aliyoyaita ni yanafanywa na watu wasiopenda ama hawana habari na Utawala wa sheria yakiwemo kuwazika watu wakiwa hai, ambapo amesisitiza hali hii inaonyesha kuwepo kwa watu waliovuka kiwango cha ukatiri katika jamii.

amesema hali ya kushamiri mauaji wilaya za Mbozi  na Momba kuhaonyesha namna jamii na watu wenye tabia kama za mshitakiwa wasivyopaswa kuvumilika mbele ya sheria na kwamba adhabu hiyo itasaidia kuwaelimisha wengine wenye mitazamo kama ya mshtakiwa Peter Mwafrika.
https://mail.google.com/mail/images/cleardot.gif