Oct 11, 2013

WATOA HUDUMA MAJUMBANI WAWEZESHWA BAISKELI ILI KUWAFIKIA WATEJA

MRATIBU WA UKIMWI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI OSCAR MGANI AKIWASILISHA TAARIFA YA MPANGO WA HUDUMA MAJUMBANI KWA WATU WANAOISHI NA VVU  MBELE YA MKUU WA WILAYA YA MBOZI DR KADEGHE
MKUU WA WILAYA YA MBOZI AKIZUNGUMZA KWENYE MAKABIDHIANO YA BAISKELI 16 KWA WAWEZESHAJI WA MPANGO WA HUDUMA ZA WAGONJWA MAJUMBANI KWA KUNDI LA WANAOISHI NA VVU IKIWA NI SEHEMU YA MSAADA WA KITENGO CHA KUDHIBITI UKIMWI CHA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI KWA MWAKA 2013/2014


Mmoja wa wanufaika wa mpango huo akikabidhiwa Baiskeli ikiwa ni sehemu ya msaada wa kuwawezesha kuwatembelea wateja wao majumbani, kwa  ujumla huduma za wagonjwa majumbani zimeonyesha kuongeza na kuchangia kuimarika kwa afya miongoni mwa watu wanaoishi na VVU hasa kutokana na msaada wa kisaikolojia ambao wamekuwa wakiukosa pamoja na ushauri kutoka kwa ndugu kutokana na hali ya unyanyapaa inayoendelea kwenye jamii zetu
Watoa huduma wakiwa wamejipanga kwaajili ya kupokea baiskeli zilizopo mbele yao
Mmoja wa watoa huduma akifurahia baiskeli aliyokabidhiwa katikati ni mratibu wa Ukimwi  wilaya ya Mbozi Oscar Mgani